Happy birthday Ben Saanane

Noel Shao

Member
Joined
Jan 19, 2017
Posts
89
Reaction score
185
HAPPY BIRTHDAY BEN SAANANE,.

Ni mwaka mmoja na siku kadhaa tangia Ben Saanane atoweke/atoweshwe katika mazingira tatanishi.
Leo Ben, anamitiza miaka kadhaa tangia kuzaliwa kwake. Happy beloved birthday bro, hero and comrade!

Naelewa namna Baba, Mama, dada, kaka na ndugu zako wanavyo jisikia, ulikuwa kaka mkubwa, lango la familia, tegemeo, ulikuwa sehemu ya furaha ya familia, Leo walio kulea wanaumia, walitamani siku ya leo mshereheke siku hii pamoja, ila imekuwa tofauti, siku imekuwa ya mawazo na mateso kuliko tegemeo.

Masonokeno na Maumivu yao tumeyaishi, machozi katika mioyo yao hayakuwahi kauka, furaha yao imekuwa ya msimu, kila wakijaribu kupata furaha, kukosenaka kwako kunaondosha furaha yao. Hakika furaha yetu itaendelea kuwa ya msimu, mpaka nyakati zile tutapo jua nini hatima yako. Uchungu tunao uishi ungepimika ungekuwa mzito kuliko mchaga wa baharini.
Angalau ingekuwa msiba tungesha omboleza yakaisha ila kwa namna ulivyo toweshwa, mioyo yetu inazidi kuchoka.
Wenye viburi vya uzima wanatunyanyasa, baba na mama nao wanaona giza, wanaumia marafiki na ndugu zako hali zao haziyumkiniki, hawaoni tumaini, Ni kipindi kigumu katika historia ya familia ya mzee Focus.

Ila katika yote, hatutakata tamaa, tupiga moyo konde, hata maandiko yanasema "duniani Kuna dhiki kubwa, ila jipeni moyo " Tutakaza moyo, tunaye MUNGU, yamkini ndiye aliye yaruhusu haya.

[HASHTAG]#Happybirthday[/HASHTAG]
[HASHTAG]#WeMissYouBenSaanane[/HASHTAG]

Happy beloved birthday, Ben Saanane.

Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
 
Sad so sad. HBD Mkuu I hope you’re still alive although it is more than one year and your whereabouts is still unknown.
 
Boss Noel C Shao Hivi hakuna taarifa ya Polisi so far iliyotolewa??? !!! Happy Birthday Mtanzania Ben Saanane.


 
Binafsi moyo unaniuma sana kila nionapp na kumkumbuka Ben Saanane, anyway ni mola tu ajuaye aliso
 
Tanzania ya leo inasikitisha sana..
Kutekana na Risasi.
HBD Brother Ben Saanane..
Ee Mungu Baba Hebu Mlinde huyu kiumbe wako Ben Saanane.

(yule Mwandishi wa Mwananchi aliyetekwa nae sijui vipi..! Ptuuu Utawala wa Shetani huu)
 
Tarehe kama ya leo 13/12 stasahau katika kumbukumbu zangu maana tarehe kama hii alizaliwa mwanaharakati ambaye amepotea katika mazngira ya kutatanisha BEN RABIU SAANANE

HAPPY BDAY KWAKO japo tuko katika kiza tororo kuhusu kutoonekana kwako,,
 
Heri ya Kuzaliwa, ila tunashindwa kusema R.I.P au tuendelee kukusubiri utarudi ulipoenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…