Happy Birthday GENTAMYCINE

Happy Birthday GENTAMYCINE

karibu tena rafiki yangu , maji ya mende wapi nije kunywa sikumwagii

Nimeamua tu kuisheherekea Birthday yangu leo kwa kutiririka sana humu JF na ningojee tu Shemela wako akirejea kutoka mzigoni tupambe na tusheherekee nae Kibaiolojia zaidi ikibidi leo safari yake ya kubeba GENTAMYCINE jr tumboni mwake ianze rasmi.
 
okey that good kifo cha mende kitaleta matunda mazuri kitu kinaenda moja kwa moja
 
Mkuu happy birthday japo ungetisha zaidi kwa kurushia na tupicha tuone umekata keki na kina nani[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]

Keki yangu nitaikatia pale Viwanjani Protea Courtyard Saa 8 hivyo hakikisheni nyote mnakuja na Bastola zenu tafadhali.
 
okey that good kifo cha mende kitaleta matunda mazuri kitu kinaenda moja kwa moja

Ha ha ha ha ha ha ha ........ Dada yangu Wewe huna adabu kweli! au unamuonea Wivu Wifi yako kuwa leo atapata burudani mubashara na pengine labda unataka kumpindua Kiaina?
 
Ha ha ha ha ha ha ha ........ Dada yangu Wewe huna adabu kweli! au unamuonea Wivu Wifi yako kuwa leo atapata burudani mubashara na pengine labda unataka kumpindua Kiaina?
hapana kaka sina nia hiyo natamani kuitwa anti mapema sasa ukianza na chuma mboga hapo ngumu sana kunasa
 
Hii ni fursa kwa wale wanaomtafuta huyu jamaa kwa sababu ya kupenda kuwazingua watu hapa jf, sasa angalieni ni mwanahabari gani maarufu ambaye siku ya leo ni birthday yake halafu mtujulishe huyu jamaa ni nani.

Cc: Nifah
 
Ofisini kwangu sio mbali na protea ntajongea kama harmorapa

Ha ha ha ha ha ha ha ...... Mkuu nakuomba usisahau pia kuongozana na Maulid Baraka Kitenge ili mnipe ushirikiano wenu wa kutukuka.
 
Ha ha ha ha ha ha ha ...... Mkuu nakuomba usisahau pia kuongozana na Maulid Baraka Kitenge ili mnipe ushirikiano wenu wa kutukuka.
Wote tuko ukanda mmoja ofisi za efm mpaka protea ukidrive Bila foleni 10 minutes so kitenge tutamtonya noma likianza
 
Happy Birthday Mkuu, Mungu akujalie maisha marefu na mazuri mbeleni.

Hata hivyo nasubiri ahadi yako uliyotoa siku ya Kuzaliwa ya Nifah kuwa utaacha upashkuna, kujidai, kujisikia na utakuwa GENTAMYCINE mpya kabisa mwenye kuleta nyuzi na comments zenye kujenga na kuburudisha.
 
Hii ni fursa kwa wale wanaomtafuta huyu jamaa kwa sababu ya kupenda kuwazingua watu hapa jf, sasa angalieni ni mwanahabari gani maarufu ambaye siku ya leo ni birthday yake halafu mtujulishe huyu jamaa ni nani.

Cc: Nifah

Usijikite sana kutaka kunijua Mimi ni nani kwani sidhani hata kama ukinijua itakusaidia kukuboreshea maisha yako au pengine labda na Wewe utapata Cheo Serikalini bali jikite mno katika kuyaelewa yale ambayo huwa nayaleta humu. Halafu nikusaidie tu Mkuu hizi ID zisikudanganye kwani unaweza ukadhani huyu ni fulani kumbe ukaja kukuta ni Mtu mwingine kabisa na ukija kukutana nae au kuambiwa hutaamini. Kipaji nilichobarikiwa ni kujua kucheza na akili za Watu na kuwapeleka vile nitakavyo halafu ni Mjanja hadi najishangaa.

Kwa faida yako tu labda nikusaidie ili nikutoe hofu Mimi GENTAMYCINE majina yangu kamili na ambayo sijawahi kuficha humu JF siku zote Watu wakitaka kunijua ni Kalemera Rwigyema Mazimpaka ni Raia halisi wa nchini Rwanda, naishi katika Mkoa maarufu na ambao ametokea pia Mchezaji maridadi kabisa wa Yanga FC Haruna Fadhili Hakizimana Niyonzima ' Fabregas ' au ' Niyo ' uitwao Gisenyi.

Elimu yangu ni darasa la Saba ( 7 ) na sikubahatika kuendelea na masomo ya juu hivyo nikaamua kujikita sana katika shughuli za Ukulima, Uvuvi na Ufugaji na ambazo Kimsingi ndizo zinaniweka hapa mjini. Tanzania ni nchi ambayo nipo tokea mwaka 1983 na huwa nakuwa hapa mara kwa mara kwa shughuli zangu MAALUM ambazo hata hivyo sidhani kama zitakusaidia mno kuzijua sana sana pengine zinaweza zikakuogofya tu.

Karibu sana Rwanda Mkuu na nategemea kusafiri wiki hii kwenda Kwetu Gisenyi kuwahi msimu wa Mavuno ambapo huwa nayapelekea pia nchini Uganda na Congo DR kwa mauzo.

Ni matumaini yangu makubwa kabisa kuwa leo angalau sasa kwa ufafanuzi huu Kuntu kabisa utaweza kuwa na amani nami.
 
Back
Top Bottom