Hey Sister,
Najua hunifahamu hata kidogo. Na kwa sasa nisingependa unifahamu. Ila ukiiona hii sentensi huenda ukapata walau picha 'HATA SASA MUNGU ANAKUTENDEA" .
You're one in a Billion. You're so kind. Kila kitu kinaweza kuwa fake JF. Ila kitu kimoja nilicho na uhakika nacho ni kuwa jina lako linasadifu yaliyomo. Wewe umetumwa kutoka Mbinguni kwa ajili ya watu wengine, mimi nikiwa mmoja wao.
HS,
Kwa leo ifurahie siku yako ya kuzaliwa, na tumuombee Mzee wetu aendelee kupumzika kwa amani. Mungu alimpa uwezo wa kumleta mtoto duniani, ambaye kwa hakika amekuwa msaada kwa sehemu kubwa ya watu.
Mungu akuhalie moyo huo huo wa kipekee.
Ipo siku nitaleta uzi kukuhusu. Na kichwa kinaweza kuwa kama ambavyo nimekiandika hapo juu. Inaweza isiwe mwaka huu au mwaka ujao, ila kwa hakika nitafanya hivyo kabla ya siku zangu kuisha.
Enjoy Sisy F 🥰
Heaven Sent