Happy birthday ibra87

Happy birthday ibra87

Namshukuru Mungu kwa Kunifikisha Siku Ya leo. Siku ambayo ni maalum kwangu. Siku Ambayo kwa mapenzi Yake yeye Mwenyezi Mungu Ibra87 natimiza Miaka Kadhaa.

Ninayofuraha kubwa kufika Siku Ya leo.. Siku Ambayo niwengi walihitaji kufika Lakini Kwa Mapenzi Ya Mungu Hawakufanikiwa Kuiona..

Ni wengi Ambao walihitaji kufurahia Siku Ya Leo lakini kwa mapenzi ya Mungu wapo kitandani kwa Sababu ya maradhi ya Hapa na Pale.

Nakushukuru Mungu kwa Mapenzi Yako kwangu.... Bila wewe ibra nisingekuwa hapa..

Nawashukuru Wazazi Wangu Mwahija Hussein Mganga na Dk Haji Masimba kwa kunilea na Kunikuza mpaka leo hii nimekuwa Hivi.. Nawapenda Sana Wazazi Wangu na nitawapenda milele.

Watoto Wangu Christina Masimba Na Yasser Masimba nawapenda Sana Watoto Wangu. Siwezi kuongea Mengi sana lakini tambueni kuwa baba Yenu ninawapenda na Kuwakumbuka Sana... Natamani Mngekuwepo Hapa nilipo ili mnifariji na Kunitia Nguvu lakini Hampo karibu. Nawapenda Sana tena Sana.

Wanajf Wenzangu na Wale wote ambao wanaadhimisha Siku yao ya Kuzaliwa kama Mimi nasema HAPPY BIRTHDAY..

Ahsanteni sana na Mungu Awabariki....

HAPPY BIRTHDAY IBRA87

Happybiday ibra Mungu akuzidishie miaka mia mingine uone wajukuu mpka vilembwe
 
Happy Birthday broh...hv a looong life.
 
Back
Top Bottom