Happy Birthday, Mr President na Penzi zito la Marilyn Monroe kwa Rais Kennedy

Happy Birthday, Mr President na Penzi zito la Marilyn Monroe kwa Rais Kennedy

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Usiku wa jumamosi ya tarehe 19 Mei, 1962, katika ukumbi wa Madison Square Garden, New York, uligeuka kuwa jukwaa la historia ambalo halitokuja kuandikwa vizuri hata kidogo katika siasa na burudani ndani ya Taifa la Marekani.
images (39).jpeg

Ni usiku ambao Marilyn Monroe, mrembo mwenye mvuto wa kipekee, aliimba wimbo wake wa “Happy Birthday, Mr. President” kwa sauti yenye mahaba mazito na moyo uliojaa bashasha, wimbo huu ulibeba ujumbe mzito sana ambao watu kama Adlai Stevenson, na Greta Garbo na wengine waliona kama burudani.
images (40).jpeg

Ila kwa Robert F. Kennedy, Peter Lawford pamoja na Danny Kaye walitambua kuwa huu wimbo ni zaidi ya burudani bali ni salamu za mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanadada Marilyn Monroe kwenda kwa Rais John F. Kennedy.
images (41).jpeg

Usiku huo ulihudhuriwa na watu takribani 15,000, na sio wazamiaji bali wageni wenye heshima kubwa sana, fikiria shughuli ya kukaribisha siku kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Rais tena wa Marekani. Usiku huo ulibeba mambo makuu mawili, moja ni show kababe ambayo Monroe alionesha mbele ya wageni, ila kubwa zaidi mara baada ya kuimba wimbo wake huo wa “Happy Birthday, Mr. President”.
images (42).jpeg

Wimbo huu ndio ikawa ni taa ya kijani kuwa Rais John F. Kennedy anatoka kimapenzi na Marilyn Monroe na ikatosha kumpa wasiwasi mkubwa sana Jacqueline Kennedy ambaye aliingia baridi kuona tetesi kuwa Mumewe ana uhusiano wa kimapenzi na **Monroe.
images (43).jpeg

Monroe hakuwa mwanamuziki wa kawaida, sauti yake ilikuwa ni tamu kusikiliza kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Alijulikana kama nembo ya uzuri na uzuri wake ulikuwa wa kuvutia kila mmoja, kuna wakati mpaka wapiga picha walikuwa wakishindwa kufanya kazi kwani uzuri wake ulikuwa sio wa kawaida hata kidogo. Lakini nyuma ya tabasamu lake na sauti tamu ya mahaba, Monroe alikuwa mwanamke aliyekumbwa na huzuni sana, upweke na kiu ya kupata mtu wa kumpenda.
images (44).jpeg

Mhusika mkuu wa kumaliza kiu hii, kama inavyodokezwa na kitabu cha “An Unfinished Life: John F. Kennedy, 1917–1963” kutoka kwa Robert Dallek, alikuwa Rais wa Marekani mwenye haiba ya kipekee Bwana Mkubwa John Fitzgerald Kennedy.
images (46).jpeg

Monroe aliingia jukwaani akiwa amevaa gauni la kung’aa lililotengenezwa kwa vitambaa vyembamba sana kiasi kwamba ilionekana kama ngozi yake, nguo hiyo haikuwa nguo ya kawaida, bali gauni hilo lilikuwa ni kazi bora sana kutoka kwa Jean Louis. Baadhinya ripoti zinadai Monroe hakuwa amevaa bra wala underwear usiku huo.
images (47).jpeg

Alipotamka maneno “Happy Birthday, Mr. President…”, ukumbi ulitulia ni kama vile ndani ya ukumbi wa Madison Square Garden kulikuwa na watu wawili, yeye pamoja na Rais John Kennedy, ukiachana na mashairi nyuma ya sauti hiyo ya mahaba, kulikuwa na hisia nzito, zilizozidi burudani. Kulikuwa na ujumbe wa upendo, wa hali ya juu. Huu ndio ulikuwa mtindo wa Monroe wa kuwasiliana na mwanaume aliyemchoma moyo wake – Rais wa taifa la Marekani.
images (42).jpeg

Seymour Hersh katika kitabu chake “The Dark Side of Camelot”, alionesha madai kuwa uhusiano wa Monroe na Rais John Kennedy. haukuwa siri ndani ya duru za kisiasa. Viongozi wa usalama walihofia kwamba ukaribu wao ungeweza kupelekea hatari kwa usalama wa taifa.
images (45).jpeg

Wakati Monroe alipokuwa karibu na familia ya Rais Kennedy, kulikuwa na hofu kwamba angeweza kuvujisha siri za kitaifa – ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya – kutokana na mapenzi yake na Rais Kennedy.
images (40).jpeg

Ni jambo la ajabu na lenye kushangaza lakini si geni kwa viongozi wa juu kuwa na mahusiano ya kimapenzi ya pembeni. Vitabu kama “All the President’s Women” na “First Women: The Grace and Power of America’s Modern First Ladies” vinafafanua jinsi baadhi ya Marais wa Marekani walivyohusishwa na wanawake tofauti nje ya ndoa zao.

Lakini kile kilichotokea kati ya Monroe na Rais Kennedy kilikuwa cha kipekee kwa sababu ya umaarufu wa Monroe na ukimya wa serikali juu ya suala hilo.
images (48).jpeg

Baada ya tukio hilo la Mei 1962, hali ya Monroe ilibadilika haraka. Alianza kuwa na huzuni, na hisia za kutengwa. Alikuwa akifuatiliwa na maofisa wa FBI na CIA kila sehemu, hali iliyomwongezea wasiwasi. Hata alipokuwa akienda kupumzika Palm Springs pale California ilikuwa ni rahisi kuona maafisa usalama wakimfuatilia.
images (40).jpeg

Bi mdada alilewa mahaba kiasi cha kushindwa kwenda kufanya kazi tena, Monroe akitakiwa kuwepo kwenye uchukuaji wa picha kwa ajili ya filamu ya Something’s Got to Give na chelewa chelewa zake ziliongeza bajeti.

Hivyo Juni 8 Kampuni ya 20th Century Fox ikamua kuvunja mkataba na kumtimua Monroe kwa kosa la kutokufika kazini huku pia tukio la kuimba wimbo wa “Happy Birthday, Mr. President” likiwa ni msumari wa mwisho ambao 20th Century Fox waliona utawachafua zaidi.
images (39).jpeg

Mnamo Agosti 5, 1962, mwili wa Marilyn Monroe ulipatikana katika chumba chake mjini Los Angeles. Taarifa rasmi zinasema alikufa kwa kutumia dawa kupita kiasi (overdose). Lakini mpaka leo, kuna maswali yasiyo na majibu. Je, aliuawa ili kuficha uhusiano wake na Kennedy? Je, alikuwa na taarifa za usalama wa taifa alizotishia kuzitoa?
images (45).jpeg

Waandishi Donald Wolfe na kitabu chake cha “The Last Days of Marilyn Monroe” pamoja na Anthony Summers katika kitabu chake cha*“Goddess: The Secret Lives of Marilyn Monroe”, hawa wawili wameonesha wasiwasi na kudai kuna uwezekano mkubwa kwamba *Monroe aliuawa kwa sababu alihatarisha hadhi na usalama wa familia ya Rais Kennedy.
p.22-2a8e25d.jpg

Kwa mujibu wa ripoti kadhaa, inadaiwa kuwa Mwanadada Monroe alikutana na timu ya maafisa usalama wa juu kutoka FBI na CIA mara kadhaa na alipewa maelekezo kuwa aachane kabisa na akae mbali na Rais Kennedy, na familia nzima ya Rais Kennedy mapenzi yakawa mazito na alikaidi.
images (40).jpeg

Kifo cha Monroe kimeendelea kuwa fumbo kubwa katika historia ya Marekani. Lakini kinachojulikana ni kwamba uhusiano wake na Rais Kennedy uliweka historia mpya ya jinsi maisha ya viongozi wa kisiasa yanavyoweza kugusa – na kuharibu – maisha ya watu wa kawaida, hata wale maarufu kama Monroe.

Leo, tunapoitazama ile video ya “Happy Birthday, Mr. President,” wengi huona kama ni kipande cha sanaa na burudani. Lakini kwa jicho la undani, kilikuwa ni kilio cha mapenzi kilichojaa huzuni, matumaini yaliyokufa, na tahadhari ya hatari ambayo mara kadhaa hutokea endapo mtu atachanganya siasa, mapenzi na usalama wa taifa.
images (46).jpeg

Historia ya Marilyn Monroe na Rais Kennedy inatufundisha kuwa maisha ya viongozi wa kisiasa ni ya hatari si kwao tu, bali kwa wale wanaoguswa nao kimapenzi. Katika dunia ya siasa, mapenzi yanaweza kuwa tishio la kitaifa.
images (47).jpeg

Kuna familia za kuweka mahaba nazo na kuna familia ambazo mtoto wao akikupenda ni sawa na kuwa kwenye orodha ya FBI: The Most Wanted.
images (48).jpeg

Kaka ukipendwa na binti wa Rais wa Marekani ama Urusi ukafanya ujinga basi ni kama wewe upo nafasi ya Ryan James Wedding, na dada ukikamata moyo wa kijana wa Rais wa Urusi ama Marekani ukampiga matukio ni sawa na kuwa kwenye nafasi ya **Ruja Ignatova.

Goodbye Norma Jeane, Though I never knew you at all
You had the grace to hold yourself, While those around you crawled.
 
Back
Top Bottom