Dhamana ya uongozi haikufanyi wewe uwe ni mtu zaidi ya raia wengine wowote waliopo pale. Haikufanyi wewe uwe na haki zaidi kuliko mtu mwingine ambaye si kiongozi. Anao wajibu wake wa uongozi kwako na wewe unao wajibu wako kwa kiongozi wako," alisema Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Kikwete aliongeza kwa kusema, "Na hili ni jambo kubwa kwa viongozi kutambua kwamba kujishusha hakukufanyi usiwe kiongozi. Kujimwambafai (kujifanya mwamba) hivi wala hakukufanyi uwe kiongozi zaidi. Una wakati wa kutekeleza majukumu yako lakini unapokuwa na binadamu wenzako ni wanadamu kama wewe.
Happy birthday mwasiasa uliekuja kitofauti zama zako.