Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,595
AFRICA ILIPOISHANGAZA DUNIA
Sasa ni zamu ya kushabikia teams zetu za Africa maana tulifanikiwa katika miaka kudhaa nyuma na kuishangaza dunia.
Ikumbukwe kombe la dunia la mwaka 1998 liliisha kwa aibu kwa team kubwa na mabingwa mara nyingi BRAZILI kuambulia kipigo cha mbwa mwitu katika mchezo wa fainali na FRANCE ..
UFARANSA walikuwa ni better sana kwa mchezaji mmoja mmoja ila Brazil walikuwa best....
Kwa wale tuliokuwa wakubwa mwaka 98 hatuwezi isahau ile fainali iliyosababisha vilio na majonzi dunia nzima ispokuwa UFARANSA tu..
Pamoja na BRAZILI kufungwa Goals 3 kwa 0 still walicheza mchezo uliovutia na kuamini sasa goals zinaanza kurudi..
KIKOSI CHA BRAZIL Kiliundwa na wachezaji wafuatao:
GK 1 Claudio Taffarel
RB 2 Cafu
CB 3 Aldair
CB 4 Junior Baiano YC 33'
LB 6 Roberto Carlos
CM 5 César Sampaio
CM 8 Dunga (c)
AM 10 Rivaldo
AM 18 Leonardo
CF 20 Bebeto
CF 9 Ronaldo
Substitutes:
MF 19 Denílson
FW 21 Edmundo
KIKOSI CHA UFARANSA kiliundwa na Magwiji wafuatao:
GK 16 Fabien Barthez
RB 15 Lilian Thuram
CB 18 Frank Leboeuf
CB 8 Marcel Desailly
LB 3 Bixente Lizarazu
DM 7 Didier Deschamps (c) (KOCHA WA SASA WA UFARANSA)
CM 19 Christian Karembeu
CM 17 Emmanuel Petit
AM 10 Zinedine Zidane
AM 6 Youri Djorkaeff
CF 9 Stéphane Guivarc'h
Substitutes:
MF 14 Alain Boghossian
FW 21 Christophe Dugarry
MF 4 Patrick Vieira
Na mchezaji wa UFARANSA Zinedine Zidane akawa mchezaji bora wa Dunia-1998
WAAFRICA WALIPOISHANGAZA DUNIA MWAKA 2002-KOMBE LA DUNIA
Ukitoa mastaa hawa wote wa UFARANSA ila waafrica tulikuwa na spirit ya hali ya juu tukiwakilishwa vema na nyota wetu waliopo SENEGAL.
Mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia 2002 kule KOREA na JAPAN ilikuwani bingwa mtetezi UFARANSA na Team ya AFRICA,SENEGAL .
Dunia nzima ikajua kabisa ni muda sasa wa kwenda kuhesabu magoli ya UFARANSA maana mategemeo yote duniani ni kuwa mwafrika kaingia choo cha kike .
Kikosi cha UFARANSA kilikuwa kile kile ukiongeza na mtaalamu THIERRY HENRY(hahaha fundi nae aliitwa) hivyo kifo cha waafrika SENEGAL kilikuwa hakikwepeki machoni mwa wapenda SOKA duniani KOTE .
Senegal kwa spirit ya hali ya juu walikuwa na kikosi kifuatacho:
1. Sylva
2 .Daf
3 .Sarr
4 .Malick Diop
5 .N'Dour
6 .Cissé (c)
7 .H. Camara
8 .Traoré
9 .S. Camara
10. Fadiga
11 .Diouf
12 .Faye
13 .Diatta
14 .Mo. N'Diaye
15 .Diao
16 .Diallo
17 .Coly
18 .Thiaw
19 .Bouba Diop
20 S. N'Diaye
21 ..Beye
22 .Cissokho
23 .M.a. N'Diaye
Hiko kikosi ndio kilichotuvurumua KICHWA CHA MWENDAWAZIMU (4-1) mwaka 2006(if I not mistaken) hivyo napotaja majina kama Henry Camara najua wasukuma wa CCM KIRUMBA wanayajua vizuri kabisa na wengine waliona LIVE goli la kichwa la Mo.N'Diaye
TURUDI KWENYE MADA :
Kama nilivyosema kuwa dunia nzima ikaamini sasa ni mauaji kwa waafrica wanaocheza na bingwa mtetezi
Mechi ya kwanza GROUP A Ni Senegal Vs France ,bingwa mtetezi .
Ni mechi iliyochezwa siku kama ya leo ya 31/5/2002 hivyo naweza isema kama HAPPY BIRTHDAY SENEGAL.
SENEGAL waliingia uwanjani wakijua kabisa KICHWA cha ZIDANE kinapiga SHUTI sawa na mguu hivyo kichwa chake ni kalali yetu.Fomula ni moja AKIRUKA JUU BASI WEE RUKA ZAIDI YAKE
Hatimaye refa aitwaye Ali Bujsaim wa UAE akapuliza kipenga kuharaisha mauaji ya waafika watakayokutana nayo kutoka kwa maroboti wa FRANCE.
Kama mnavyojua au naweza msingizia Mugabe akisema "KUISHI AFRICA NI CV PIA INATAKIWA KUANDIKWA KWENYE CV UNAPOTAKA KWENDA KUOMBA KAZI" hivyo Senegal wakijua kabisa Dunia nzima watakuwa upande wa FRANCE hivyo ni mechi kati ya Senegal na dunia nzima (hahaha hata washabiki waliokuwa nchini Senegal walishangilia FRANCE )
Hivyo naweza itaja mechi hii kama :
SENEGAL VS WORLD CUP
Waafrica,Senegal wakaibuka kwa shambulio la kushtukiza na kufanikiwa kupata goal dakika ya 30 lililofungwa na PAPA DIOP na kuinyamazisha dunia kwa dakika kadhaa..
Hivyo ubao wa matangazo kusoma hivi:
Senegal ni wa Africa kama wa Africa wengine tumeweza kuvumilia njaa,kiu ,jua ,utumwa na mateso yote hivyo ni jambo rahisi tu kuvumilia dakika 60 zilizobaki hivyo tukapaki baki ambapo basi kama lile kwasasa hakuna team inaweza kupaki(hata Mourinho wa Man Utd hajalifikia na katika historia ndio basi gumu zaidi kutokea ).
Hili ni bus ambalo waliwekewa wachezaji bora wa dunia,ambao ni hawa :
GK 16 Fabien Barthez
RB 15 Lilian Thuram
CB 18 Frank Leboeuf
CB 8 Marcel Desailly (c)
LB 3 Bixente Lizarazu
CM 4 Patrick Vieira
CM 17 Emmanuel Petit
RW 11 Sylvain Wiltord
AM 6 Youri Djorkaeff
LW 12 Thierry Henry
CF 20 David Trezeguet
Substitutions:
FW 21 Christophe Dugarry
FW 9 Djibril Cissé
Kuweza kuzuia mafuriko kwa mkono ni kitu kisichowezekana ila kama ngamia wa kwenye Biblia aliweza kupita kwenye tundu la sindani ndio hapo Senegal walipoamini kuwa yanawezekana na kupaki UKUTA ambao mpaka leo kule Ufaransa wanathubutu kusema hawajawahi ona team yao ikicheza mpira mbovu kama ule..
AFRICA (SENEGAL ) baada ya kupata goal wote tukarudi nyuma na Kuonyesha dunia namna BUS linavyopaki ,na kocha wa MAN U ,Mournho akaiga BUS lile na kulipeleka ulaya.
Kwa spirit ile ile tuliyoanza nayo ,AFRICA tukafanikiwa kuishangaza dunia pale refa alipopuliza tena kipenga kuashiria kuwa GAME IS OVER
na haikuishia hapo tukawashangaza tena kwa kuingia ROBO FAINALI..
Na mapicha picha ya kutisha
Hivyo kwa moyo huohuo ,AFRICA tunaenda kuishangaza tena DUNIA baada ya kuwashangaza 2010 .
HAPPY BIRTHDAY SENEGAL,BEST WISHES AFRICA.
Deadbody