Umekuja kujianzishia thread humu? Msanii gani huyu analilia show, kwa nyimbo zake amuite Nani? Anasifiwa Hadi na Young lunya show zote kubwakubwa yumo
Wewe Niki ni fwala tu, watakusikiliza hukohuko buza na kwa mpalange
Sasa Afrika mikononi ukoloni ndo umeshafika ukingoni/ mboni ya msomi haitodanganyika
Nalazimika kufika nainjika chungu jikoni/ imebadilika mpaka namshika mzungu kiunoni
Waliyo hai/wanaishi kwa imani zilizokufa/
Sitaki kujenga ukuta ndiyo maana naziba nyufa/
Kaa chini vuta hisia weka umakini kisha kumbuka/ homa ya dunia soma historia kisha zinduka/
Martin Luther,
Malcolm , William true boys/
Nguzo zenye tunzo mafunzo hakuna new choice/
Ubaguzi wa rangi, dini na kabila/ tawala za kinazi ubabe nini dhamira/
Uzushi na ubaguzi wa madhehebu na vyama vya siasa/ imani za kikushi kizazi hakina darasa
Uko wapi muelekeo, mtazamo na tegemeo/ pembejeo zimeadimika na hii ndo afrika ya leo
Mwendo wa kuchechema viongozi wamechakachua/Dhamana walizopewa nkisema huenda wakaniua/
Usinitishe kwa cheche ilihali moto naujua/ Eti John Speke ziwa Victoria ndo kagundua/
Nateta na wabongo kwa Kiswahili na sio kimombo/ Afrika nitokayo mimi si ile ya Christopher Colombo/
Sio bara giza bara mama la ulimwengu/ na dhahiri kuwa utajiri wa mzungu unatoka kwetu/
Bashiri za kale kwa sasa ndiyo maisha halisi/ Watu wenye mioyo yabisi watu wenye taifa la uasisi/
Utani wa jadi
Umetupwa kando baba kapinda/ Macho kwenye pesa kama Fikiri madinda/
Wapo waliopotea kwa kumuiga Elton John/ Ndipo anapotokea naitimiliza Teflon Don/ Vuka Kibo na Mawenzi twende Elgon zone/ Uone Afrika ya leo na hii ni episode one/
Afrika ya Leo- Nikki Mbishi nyimbo ya 2008 au 2009 hiviii