Fohadi unaona jinsi unavyonitafutia Matatizo? Tayari Wapumbavu na Waswahili wenye Chuki na Wivu wa Umaarufu wangu hapa JamiiForums wameanza Kuhisi kuwa hii ID yako ni Mimi GENTAMYCINE na kwamba nimejianzishia Mwenyewe tu huu Uzi ili.kutafuta Sifa zaidi.
Tayari kuna Uzi wangu wa Kujitakia Happy Birthday Mwenyewe niliuanzisha Juzi Saa 6 na dakika 1 Usiku na bado upo nashangaa bado Watu wananihusisha Mimi na hii ID yako.
Yaani kuna Watu hapa JamiiForums wananichukia utadhani labda nimekula Chao au nina Deni nao au nimelala na Mama zao Wazazi hivyo nimewatelekeza au labda Mimi ni Kikwazo cha Kiuchumi kwa Maisha yao au labda Shida zao na Umasikini wao mkubwa ( ambao hata Mimi GENTAMYCINE ninao ) unasababishwa nami.
Na kinachonisikitisha zaidi sasa mpaka Nawadharau mno Haters na Critics wangu wengi hapa JamiiForums ni kwamba Wao ndiyo kila Uchao wanatangaza Kunichukia, Kutonipenda na hata Kuniombea nipigwe BAN tena ikiwezekana ile Permanent Ban lakini ndiyo hao hao 24/7 wakiingia hapa JamiiForums ni lazima wanisome nimeandika nini, nimechangia nini na wengine hadi Wananifolo.
Mtu haumpendi, ila Kutwa unamsoma.
Cc:
Leak