Happy born day Mwamba Mbowe

Mi nikajua we mwenyewe au baabako katimiza hiyo miaka 60,, ili tukutakie heri na baraka kumbe hawa wajasiliamali wa kisiasa agha!!!
 
Mwambieni Lisu na Lema waache kudanga Ulaya warudi Tanzania kula kwa jasho lao.

Wazazi wa mbowe wanajisikiaje kutuletea balaa la ugaidi watanzania
 
Mkewe na watoto wake sijui wapo hali gani kuona mume/baba ana sherehekea siku yake ya kuzaliwa jela. Tena kwa tuhuma za kusingiziwa


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Tuwaweke kwenye maombi, sio jambo rahisi
 
Yeah, Mbowe anakula pesa za chama, Segerea! Una akili kubwa sana mkuu!
 
Huyu siyo ccm tu, ni sukumagang mjinga! Achana na mjane mkuu, hawezi kukuelewa!
 
eh MANENO MAKALI HAYO BRO
 
Tangu kuanza kwa upinzani rasmi 1995, ccm huwa wako makini kumtarget mtu au watu au taasisi ambayo ina uungwaji mkono mkubwa na watanzania, dhidi ya serikali zake za kibaradhuli. Mwaka 1995, baada ya Agustino Mrema kujiengua ccm na kujiunga NCCR, nchi ilizizima, na Mrema mara moja akawa mlengwa. Kila mara alipigwa mabomu ya machozi, na NCCR ikalengwa kwa njama za kila aina. Baada ya NCCR kuporomoka, CUF ndio ikawa namba moja katika upinzani. Mara ooohhh, chama cha waarabu. Mara ooohh, watamleta sultani, na propaganda kemkem. Lipumba alishambuliwa na polisi mara kwa mara wakati huo.
Kipindi chote hicho, CHADEMA walikuwa wapo, lakini ccm wala hawakuwa na habari CHADEMA ni kitu gani. Taratibu CHADEMA ilipata wabunge wengi zaidi kila uchaguzi. Kufika 2010, CHADEMA ilipomsimamisha dokta Slaa kugombea urais, hapoooo, mizinga ya ccm ikaelekezwa kwao. Mara ooohhh, chama cha wakristu. Sasa CHADEMA ndio chama kinachoisumbua ccm. Uchaguzi wa 2015 ccm ilipigwa chini, lakini kwa kufuata mila chafu na najisi, iliyoasisiwa na Nyerere tangu uchaguzi wa 1995, pale alipomlazimisha komandoo Salmin Amour ambaye alishatundika buti baada ya kushindwa na CUF ya maalim seif, abaki madarakani. Tokea hapo ccm wanajua hakuna mungine, ni wao tu hata kama wananchi watawakataa kwenye kura.
Kwa kutazama tu kampeni za CHADEMA 2020, ni wazi CHADEMA ndio chaguo la watanzania walio wengi. Pamoja na hujuma za serikali ya ccm, jinsi muda ulivyokuwa unakwenda, ndivyo wengi zaidi walielewa ujumbe wa mgombea wa CHADEMA , na ndivyo serikali ya ccm ilivyozidi kuchanganyikiwa, na hatimaye kufanya uporaji wa kihistoria.

Mbowe, kama ilivyokuwa Mandela, anabeba matumaini ya wengi. Haina maana wengine hawapo. Wapo kina Lissu, kina Lema, kina Msigwa, kina Heche, na wengine wengi. Ila kiukweli, jinsi ccm wanavyotumia nguvu dhidi ya Mbowe, ndio wanazidi kumpaisha.
Kumbuka pia Mbowe ni mtu wa pekee. Ameitoa CHADEMA chini na kuileta juu. Na kwa kuwa serikali ya ccm wanajua fika kwamba Mbowe ndio kaibeba CHADEMA hata kifedha, waliamua kumsambaratisha kiuchumi. Akaunti zake zote zilifungwa na Magufuli. Miradi yake ikahujumiwa. Bado jamaa wanachanja mbuga. Mwishowe wamekuja na mkakativwa kumfungulia kesi ya ugaidi. Wataweza kumdhibiti mpambanaji huyu ? Asilani hawawezi! Toka lini majambazi, wezi, waporaji wakashinda?
 
Matumaini ya Watanzania wanabebwa na Watanzania wenyewe. Mbowe pekee hawezi kubeba matumaini ya Watanzania. Tatizo hapa ni kumuweka mtu mmoja juu ya wengine anaofanya nao kazi.
Ni kweli Mbowe peke yake hawezi kufanya chochote. Lakini nguvu ya Mbowe, inayofanya serikali ya ccm ijiharishie, inayofanya hata mabalozi wa nje wanafuatilia kesi yake, ni kutokana na nguvu ya umma. Na nguvu hii haipatikani kimchezo. Ni kutokana na kujitoa muhanga kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Mbowe ni iconic figure. Ni kama akina Yasser Arafat. Watu aina hiyo wanatengenezwa kwa kuvumilia mateso, vifungo vya magerezani, manyanyaso, nk. Wananchi hatuteswi, anaandamwa Mbowe. Ndio maana ni yeye anayepata heshima hii
 
Yaani tunakuwa na cultish belief kwamba hakuna mwingine isipokuwa yeye.
Hayo ya "cult" yalikuwa ya Magu. Huyu alitaka asifiwe na kuabudiwa. Kwa Mbowe ni mateso, vipigo, kesi kila uchao. Bila shaka watanzania wanajua kwamba huo ni uonevu, na ndio maana anapata sympathy yao. Ccm wanataka aonekane mhalifu. Lakini mtu mhalifu mbona anajulikana sana tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…