Happy Mariage Day:- Njooni tuwape pole waliojitafutia majanga makuu kwenye hii dunia ya utandawazi..!!!

Happy Mariage Day:- Njooni tuwape pole waliojitafutia majanga makuu kwenye hii dunia ya utandawazi..!!!

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
6,958
Reaction score
16,358

Siku ya Kimataifa ya Wenzi wa Ndoa:kuheshimu mume na mke kama msingi wa familia​

Siku ya kimataifa ya Wenzi wa Ndoa ni sheherehe ambayo inahimiza kuheshimu mume na mke kama jiwe kuu la pembeni la familia,umoja msingi wa jamii ya kila tamaduni,kabila,koo na taifa.Adhimisho hili linahamasisha uzuri wa uaminifu wa ndoa na maana yake kama sadaka na furaha ya maisha ya ndoa kila siku!

Andiko Kutoka Vatican.

Siku ya Kimataifa ya Kimataifa ya Wenzi wa Ndoa ambayo uhadhimishwa kila mwaka katika Dominika ya Pili ya mwezi Februari, mwaka huu imeangukia tarehe 09 Februari 2025.
Lengo kuu kiutamaduni ni kwamba mume na mke wanaheshimiwe kama jiwe kuu la pembeni la familia, umoja msingi wa jamii kwa kila tamaduni na taifa. Adhimisho hili linakuza uzuri wa uaminifu wa ndoa na maana yake kama sadaka na furaha ya maisha ya ndoa kila siku. Kutokana na hili unaweza kuelewa zaidi ni nini maana yake katika adhimisho.
Siku hii inayo adhimishwa kila mwaka katika Dominika ya Pili ya mwezi Februari, ni siku ambayo inarejesha kumbu kumbu ya Mtakatifu Valentine anaye julikana ulimwenguni kote kama mwombezi wa wanandoa au "wapendanao", ifanyikayo kila ifikapo tarehe 14 Februari.

Siku ya wenzi wa ndoa Duniani

Hii ni siku ya Wenzi wa Ndoa ili ulimwengu uweze kushuhudia kwamba licha ya matatizo mengi yanayojitokeza katika ulimwegu wa mahusiano, lakini bado kuna ndoa nyingi zenye furaha na kudumu, kwa sababu mtu anaweza kujifunza kupenda kwa dhati, kutunza mahusiano na mawasiliano, kudhibiti tofauti ambazo kila wanandoa wanazo. Kwa ufupi ni kwamba kufurahia maisha kama wanandoa ni kitu ambacho kweli unaweza kujifunza na kutimizwa. Na ndiyo upendo wa maisha ambao unawezekana! Ni siku ya heshima kwa waliooana karibuni, wa zamani, na watarajiwa kama njia ya kuanzisha familia na kuleta jamii pamoja kila wakati.

Historia ya kuadhimisha siku hii ilianzia huko Louisiana Marekani

Wazo hili la kusherehekea siku ya Wenzi wa Ndoa lilianzia huko Louisiana, mnamo mwaka wa 1982. Kundi la wanandoa wanaolingana walimwomba meya wa jiji, kwa Askofu, na gavana wa Serikali hiyo kutangaza Siku ya Mtakatifu Valentine iitwayo 'Wapendanao', kama siku ya “Tunaamini katika ndoa”. Tukio hilo lilifaulu, kwa hiyo wazo hilo liliwasilishwa katika Bodi ya Kitaifa ya Marekani ya Mkutano wa Wenzi wa Ndoa Ulimwenguni pote, ambayo ilikubali ili kupandishwa cheo. Na mnamo mwaka uliofuata, 1982, magavana 43 walitangaza rasmi Siku hiyo, na sherehe hizo zilifikia hata vituo vya kijeshi vya, Marekani katika nchi kadhaa. Mnamo 1983, jina lilibadilishwa na kuwa “Siku ya Wenzi wa ndoa Ulimwenguni”, ikilenga kusherehekewa katika kila Dominika ya Pili ya mwezi Februari kila mwaka. Tangu wakati huo, duniani kote, wanandoa wengi huadhimisha siku hiyo kwa njia tofauti, ambayo kimsingi inalenga kuwaheshimu wanandoa kama msingi wa familia, ambayo yenyewe ni kitengo msingi cha jamii, hasa ikiwa ni kutoa sifa ya uaminifu, kujitolea sadaka kwa mmoja na mwingine katika familia yao na kudumisha furaha ya maisha yao ya kila siku ya ndoa yao.

Pete ya harusi ni ishara ya kihisia na ya milele

Tujifunze siri ya kuvaa Pete ya harusi kwenye mkono wa kushoto hasa wale wote ambao wamefunga pingu za maisha. Miongoni mwa vifaa vyote vya wanawake na wanaume, pete ya harusi ilichaguliwa kubeba ishara ya kihisia na labda ya milele, na huleta pande mbili pamoja ili kutangaza kukaa kwao pamoja hadi mwisho. Na zaidi inaonesha uhusiano mtakatifu zaidi na wa kibinadamu katika historia, ambayo ni harusi yenyewe na wahusika Bi na Bwana Harusi. Lakini je umewahi kufikiria juu ya sababu ya uchaguzi huo wa pete ya harusi? Wazo hilo linatoka wapi na maana yake ni nini? Au ni kitu nasibu kupitishwa kutoka kizazi hadi kizazi? Pete, au pete ya duara kama ilivyoitwa, ilitumiwa kwanza kama ishara ya ndoa au kuonesha uhusiano wa watu wawili pamoja kwa maisha yote, angalau miaka 6,000 iliyopita, kulingana na na maelezo ya Business Insider. Na pete hizo zilitengenezwa kwa mwanzi au matawi ya mmea wa papyrus na zilipitishwa kutokakatika tamaduni za kale za ustaarabu wa Misri. Kwa hiyo pamoja na mengi ambayo tunayapata kutoka kwenye ustaarabu wa Misri ndugu msikilizaji kama unapenda kujifunza na udadisi zaidi ili jifunze.

Poke pete hii iwe ishara ya uaminifu wangu kwako

Ndugu msomaji wa Vatican Newes, mengine unaweza kujifunza kwa udadisi zaidi ili uweze kuwa na utambuzi mwingi tu. Kwa leo ni bora pia kuwakumbusha kwa wana Ndoa katoliki, au watarajiwa wakati wako mbele ya Altare siku ya kufunga ndoa. Na kabla ya hayo katika Kitabu cha Mwanzo kinabainisha kuwa: "Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimuumba; mwanaume na mwanamke aliwaumba. (Mwanzo 1:27). Na Padre kwa hiyo anasema: “basi kwa kuwa mwakusudia kufanya maagano ya ndoa takatifu peaneni mikono ya kuume. Na kuonesha kukubaliana kwenu mbele ya Mungu na Kanisa lake.” Kisha anaendelea: “Unampokea awe mke / mme, wako na tena waahidi kuwa mwaminifu kwake katika taabu na raha katika magonjwa na afya, umpende na kumheshimu siku zote za maisha? Jibu (kwa wote wawili) ni ndiyo. Kwa hiyo wakati wa kuvalishana pete Bi na Bwana harusi wanasema maneno haya kama kiapo: “Mwenzangu pokea pete hii iwe ishara ya upendo na uaminifu wangu kwako; kwa jina la Baba na la Mwana, na la Roho Mtakatifu”. Kwa hiyo kwa hakika hicho ni kifungo kikubwa na baadaye katika sala, Padre anaomba kuwa “Aliyekiunganishwa binadamu hasikitenganishe”. Ni mambo mazito kweli kweli. Heri ya Siku kuu ya Wenzi wa Ndoa 2025!

Credit.
Maandiko ya Vatican
 
FB_IMG_1739088319537.jpg


Dear ndugu TBC kama uko humu naomba nijibu hii picha yako kama ifuatavyo ....

Sababu ni nyepesi tu...

1. Kutapeliwa.
Wapo waliokuwa matajiri wakafunga ndoa na KUFILISIWA.

2. Mdomo.
Siwezi ishi na mtu ambaye kufunga mdomo hawezi.
Kutwaa ni kufungua mdomo tuuu hata kwa mambo ya kipuuzi.

3. Uhuru.
Mambo ya kila nikitaka kufanya kitu au kwenda sehemu nitoe taarifa HAPANA KWA KWELI.

4. Financial superman..!!
Yaani kuna raia ndoa ndio mkombozi wao wa shida zake na familia nzima.

5. Kulea watoto sio wako.
Mimi siwezi kuendekeza upuuzi wa Kitanda hakizai haramu, ni ujinga wa hali ya juuu

6. Kugongewa.
Ndio wanagongewa sanaa ila WANAVUMILIA na kufa na MAGONJWA YA MOYO.

7.....
8....
9...
10....

NARUDI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Siku ya Kimataifa ya Kimataifa ya Wenzi wa Ndoa ambayo uhadhimishwa kila mwaka katika Dominika ya Pili ya mwezi Februari, mwaka huu imeangukia tarehe 09 Februari 2025.
Lengo kuu kiutamaduni ni kwamba mume na mke wanaheshimiwe kama jiwe kuu la pembeni la familia, umoja msingi wa jamii kwa kila tamaduni na taifa.
Sawa. Ni jambo jema.
Ngoja ambao tayari wameshaingia kwenye ndoa waje.
 
Jambo jema lipi hilo???
😳😳😳

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Hili

Lengo kuu kiutamaduni ni kwamba mume na mke wanaheshimiwe kama jiwe kuu la pembeni la familia, umoja msingi wa jamii kwa kila tamaduni na taifa.
 
Tusisikilize walimwengu hawana wema hao

Hawana wema hao....

Tupatapo neno tulichuje lililo jeema

liwe letuuu

mpenzi wangu nakupentaaaaa ....

Mpenzi wangu ulivyo umbikaaaaa

katika viumbe umezidi wote

Khery kwenu wanandoa

Blood bruh ibn Unuq

Mentor Dr am 4 real PhD

Mzee wangu Etugrul Bey

BRAZA CHOGO

Mad Max

Liverpool VPN

Intelligent businessman 😂

secretarybird

bonjov bwashee

Kherini wanandoa 😝
Tupo mkuu 😊 naziona anniversary kibao za ndoa yangu.

We happy na mtoto kafanana na nani...

Ngoja niweke dedication hapaa

NADIA MUKAMI_KAI WANGU

Some of lyrics....

Mtoto anafanana na nani
Je ana macho kama Nadia Mukami
Atapenda gym kama baba yake Ali
Ndio maswali najiuliza tu kichwani
Niliposikia nakupata
Nililia machozi ya furaha
Ingawa sikuwa ready kukupata
Sina budi sasa kuitwa mama
Ila usijali

Mama yako mchapa kazi sana
Baba yako ana roho safi sana
Wazazi wako wote maarufu sana
Ee wangu ee utatesa sana
Namwita Jina Kai Kai Kai Kai wangu wee
Namwita Jina Kai Kai Kai Kai wangu wee
(Kai, kai kai,) (Kai kai kai yoyo) (oyo yoooo
 
Back
Top Bottom