Happy Sabbath

Mataifa Mimi siwajui katika muktadha huu, ila ninachojua ni kuwa wayahudi ndio waliomuua Yesu sababu mojawapo alivunja Sabato na sisi wafuasi wa Yesu hujitahidi sana kufuata nyayo zake
Kutokuelewa kwako maandiko kusikufanye useme kinyume na neno maandiko yanasema Yesu hakuwahi kutenda dhambi yoyote iweje wewe useme kinyume maana kusema aliivunja sabato ni kukiri wazi Yesu alitenda dhambi kwa kuihalifu amri yake mwenyewe amri ya nne

Wakati luka 4:16 inasema wazi ilikuwa kawaida au desturi yake kuitunza sabato na zaidi kwenda hekaluni kuabudu siku hiyo.

Shida yako huyajui maandiko na badala ya kufuata kile Yesu alichofundisha kuhusu sabato wewe unachukua uelewa wa mafarisayo na masadukayo kuhusu sabato na jinsi walivyoona kwa yale aliyotenda aliivunja sabato wakati yeye alikuwa aliwafundisha namna ya kuitunza hiyo sabato kwa namna ilivyokusudiwa
 
Isaya 66:23

Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

Wewe unaelewaje apa [emoji848]
Huo MWEZI MPYA mnasali wapi?
 
ISA. :58:13
Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;

Tunaifurahia sabato takatifu ya Bwana. Heri ya sabato wajoli wa Baba
 
happy too na kesho wote tuende kanisan huwa najisikia faraja san siku ya jumamos ila nisipo enda kusali naumia moyo
Usiache mkuu kujihudhurisha mbele za Bwana kwa sababu yoyote ile isiyo ya msingi labda ugonjwa tu ukuzidie
 
Isaya 66:23

Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

Wewe unaelewaje apa 🤔

Sabato ni siku ya kwanza ya Juma, hapo maana yake ni siku hata siku, ama ni sawa na kusema jumatatu mpaka jumatatu, pia maana ya hilo andiko sio mungu aabudiwe siku ya Sabato bali ni kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…