Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Nawatakia sikukuu njema mbarikiwe wote, msiumwe , msiwe na stress, muwe na moyo wa kusamehe, mpendwe na waume/boyfriend zenu,waume/boyfriend zenu wawasikilize, mfanikiwe katika kila jambo.kama nilisawahi kukukosea tumia hii sikukuu kunisamehe kwani some time ulikuwa ni mzaha ila mzaha ukaonekana kama ni kweli so kuwa na amani,mfanikiwe katika masomo yenu.na wale ambao bado wanatafuta nawaombea wapate watu makini ili wapendwe na kujisikia kuwa wapo duniani na wajijue kuwa wao ndio kila kitu bila wao sisi hatupo. Na wale wanaume wanaopiga wadada, wake zae au hata ma girlfriend zao nawaombea laana na kuwataka waache mara moja hii tabia popote walipo. wakae wakijua kuwa mwanamke hapigwi hata siku moja na wala hanyoshewi kidole ,mwanamke anafunguliwa mlango wa gari aingie na kutoka, mwanamke anaulizwa ulizwa na kudekekezwa,mwanamke ni kama yai linalindwa ili lisidondoke. nataka wanawake wote wajisikie kuwa tunawapenda na kama mimi binafsi na ninawaheshimu sana. na ile mijitu ambayo inawasumbua dada zetu kwenye rushwa ya ngono nawaombea wote laana, ili waache mara moja hii tabia.Dunia bila mwanamke isingekuwepo.
LOVE YOU ALL.
ITS ME
SAINT IVUGA !!


LOVE YOU ALL.
ITS ME
SAINT IVUGA !!



