Nadhani mapambano ya wanawake sio ya kutafuta nafasi za kipekee, bali ni kutafuta usawa kati ya wanawake na wanaume. Sio siri kwamba wanawake wana nyanyaswa kuliko wanaume, hasa vijijini. Kiwango cha kazi wanacho fanya wanawake ni kikubwa ila hakithaminiki kama kazi ya jamii. Ikiwa mwanaume anafanya kazi hizo hizo naonekana kua shujaa na anatambuliwa kwa njia tofauti. Wanawake wanataka nafasi yao na mchango wao katika jamii utambuliwe.
Kuna changamoto wanazo zipata wanawake ambazo zinahitaji mtazamo wa kipekee. Vitu kama maternity leave, gender based violence, equal pay, reproduction health, office space and career advancement vimekaa kumpendelea mwanaume zaidi kwa sasa, na kuna maana ya kurekebisha. Bila kuzichukulia changamoto hizo kama za wanawake kwa upekee itakua vigumu kufikia usawa.
Wanaume ndio wanafanya uonevu huo udumu. Ukichunguza matatizo ya office space utagundua watu wengi katika management ni wanaume. Sasa utajadili na nani ukitaka kubadilisha mambo? Ukichunguza sheria za reproductive health utagundua wabunge wengi ni wanaume, sasa utapitishaje sheria ya kupendekeza 'choice'? Ukitazama sheria za kazi unaona kazi zina mpaka wa ma saa (maximum hours of work per week) ila unaambiwa hizo hazihusu kazi za nyumbani ambazo mara nyingi vijijini asilimia kubwa inafanya na wanawake. Sasa wanawake peke yao wanawezaje kubdili mambo bila kujadiliana na wanaume?
Sio kwamba wanaume wana njama au mpango mkubwa wa kuwanyanyasa wanawake, sidhani. Haya mambo yametokea kwa muda mrefu na yanaonekana kua kawaida. I think it is just time for another discourse, another approach on understanding and implementing the universal declaration on human rights.
Mwali, yote uliyoyataja ni ya msingi sana kiasi kwamba nimeshindwa hata kuchagua lipi lina umuhimu zaidi, labda niongezee kidogo tu katika baadhi yao:
1. Usawa wa kazi: Sio vijijini tu bali hata mijini. Mke na mume wanatoka saa hiyo hiyo kwenda kazini, lakini mwanamke anaamka mwanzo kumtayarishia "bwana na watoto" chai. Wakati wa kutoka ofisini si hasha mwanamke kutoka mwisho kwa sababu "bosi" kalazimisha hili na lile lifanywe, lakini akifika nyumbani bado kazi zinamsubiri.
2. Kazi hiyo hiyo, mwanamke analipwa si chini ya 20% kasoro kuliko mwanamume. Nafasi nyingi za juu maofisini, idadi ya mawaziri serikalini, wabunge....wengi ni wanaume. Na ikitokea pahali mwanamke amekuwa raisi au mkuu wa shirika la kimataifa, hiyo inaanza kuwa hadithi na jambo la kupigiwa mfano. Cha ajabu, majumbani, mashuleni na vyuoni...duniani kote...wanawake ni wengi kuliko wanaume, wastani wa 60%, lakini mpaka leo hakuna bunge (nadhani) lililo na angalau 50-50% ya wanaume na wanawake.
3. Unyanayasaji wa kijinsia: Nitataja mfano wa nchi moja ninayoijua zaidi - Spain. Mwaka jana wanawake 70 waliuliwa na waume/ wapenzi wao na hakuna mwanamume hata mmoja aliyeuliwa na mwanamke. Sasa kuona takwimu kama hizi katika nchi "iliyoendelea", tuelewe katika nchi "zisizostaarabika" hali ni mbaya zaidi. Domestic Violence, ubakaji, biashara ya binadamu (kwa ngono), kufanyisha kazi watoto wadogo...ni matatizo ambayo mwanamke anakabiliana nayo popote alipo ulimwenguni.
4.Mwanmke kama chombo cha boashara: Angalia mfano matangazo ya biashara, mfano katika tangazo la gari jipya, tangazo la vyombo vya matumizi ya nyumbani...biashara haiendi kama hakuwekwa mwanamke nusu uchi. Hata kwenye masumbwi wanayopigana wanaume, wanawake nusu uchi ndio wanaonogesha shughuli.
6. Hilli la mwisho Mwali tunatafautiana kimawazo. Kwa mawazo yangu ni kuwa "
wanaume kwa makusudi kabisa wanawanyanyasa wanawake". Hata kama ni kweli kuwa haya mambo yalianzia mbali na sasa yanaonekana ya kawaida, lakini ni nani aliyeyaanzisha?
Hata hivyo, pamoja na kuwa mwanamme yuko mstari wa mbele katika kuwanyanyasa, kuwawekea vikwazo na kuwarejesha nyuma wanawake, nahisi wanawake na wao wenyewe wanachangia kuyaendeleza haya. Juzi pahali fulani katika jukwaa hili niliuliza, "inakuwaje katika jimbo la uchaguzi ambako wanawake wapiga kura ni wengi kulliko wanaume, lakini akisimama mwanamke kugombea, wanawake wanawapigia debe wanaume na hata kuwapikia majungu wanawake wenzao?"
Bado changamoto ni nyingi. Ni miaka 101 tangu kuanza kuadhimishwa rasmi siku hii. Mafanikio yamepatikana lakini bado sana kwa mwanamke kujikomboa. Ni wakati sasa kwa wanawake kusimama imara. Wasisubiri tarehe 8 Machi kupakwa mafuta kwa nyuma chupa na wanaume bali mapambano yawe ya kila siku na kila mahali - majumbani, mashuleni, maofisini, kwenye vyombo vya kutunga sheria n.k. Kuna baadhi ya nchi siku hii wanaume hawaruhusiwi kupenyeza pua zao katika maadhimisho. Vita ya kumkomboa mwanamke ianze na mwanamke mwenyewe.
UWEZO, NIA NA SABABU MNAZO.