HAPPY WOMENS DAY

HAPPY WOMENS DAY

Foxhound

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
28,710
Reaction score
76,243
Habari wanajukwaa!

Ama baada ya salamu kwa kawaida siku kama ya leo 8 March huwa nimezoea kuona watu wakianziasha mada mbali zinazowahusu akina mama na akina dada pamoja na wasichana kwa minajili ya kusherehekea siku ya wanawake duniani, ila katika mwaka huu 2020 naona hali ni tofauti na ilivyozoeleka.

Nimejaribu kupekua huku na kule lakini bila mafanikio sijakuta mada zinazowahusu.
Baadhi ya majukwaa watu wanajadili kuhusiana na video isiyofaa inayotrend mitandaoni huku majukwaa mengine wakijadili kuhusu mchezo wa Simba na Yanga. Binafsi sijafurahisha na watu kuisahau siku ya leo. Kwa kuwakumbuka wamama, wadada zetu.

MIMI NALIANZISHA
Kuna siku nilichelewa kurudi nyumbani! dingi akanikata stick nyingi sana akaniambia hakuna kula mchana! mtembezi hula miguu yake, halafu mama ndio alikua anaepua maharage jikoni na kitu cha wali kilikua tayari kinanukia hatari!! Nikasema haya bana, nikaenda kulala kwa huzuni kubwa sana huku tumbo likiunguruma kwa njaa!! watu wakala mimi nikawa najipitisha ili hata mzee anionee huruma nile lakini wap!!

Nikashangaa mama ananiita kwa Hasira, "We mpumbavu wewe kuja hapa, chukua hiyo ndoo uende ukachote maji!!" nikazidi kuumia kuona mama nae ananipa kazi na njaa yote ile!! basi nikasepa kinyonge nikiwa njiani nikahisi kwenye ndoo kuna kitu kufungua hivi nakutana na bakuli kubwa limejaa Wali namaharage

HAPPY WOMEN'S DAY!

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Jamani huo mfano ulimtokeaga kila mtu!! Kuna mjomba angu mmoja alishawahi kunihadithia kitu kama hicho
 
Jamani huo mfano ulimtokeaga kila mtu!! Kuna mjomba angu mmoja alishawahi kunihadithia kitu kama hicho
Maisha haya tunayaishi kuna vitu vingi vimetufanana, mfano ni nani kati yetu hajawahi kuchelewa kurudi shule, au hajawahi kunyimwa msosi, au hajawahi kula kula ada!

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Maisha haya tunayaishi kuna vitu vingi vimetufanana, mfano ni nani kati yetu hajawahi kuchelewa kurudi shule, au hajawahi kunyimwa msosi, au hajawahi kula kula ada!

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
Me hapa sijawahi
 
Me hapa sijawahi
Hata kurudi nyumbani na kukuta wamemaliza msosi?

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Maisha haya tunayaishi kuna vitu vingi vimetufanana, mfano ni nani kati yetu hajawahi kuchelewa kurudi shule, au hajawahi kunyimwa msosi, au hajawahi kula kula ada!

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
Kunyimwa chakula sijawhi Ila ada nmekula na pia kuchelewa kurudi nyumbani unasingizia foleni ya dar nmefanya mara nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kwa kweli
Basi itakuwa mabasi ya manjano wewe sio bure! Tuache sisi saint Kayumba [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Back
Top Bottom