Harakati Sasa Basi - Narudi Kubeba Maboksi!

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
Hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hapa nchini inazidi kuwa tete, hii ikiwa ni miaka 5 toka nirejee kwa moyo wote kuja kujenga Taifa. Pamoja na harakati zote hizo bado hali ya umaskini inadhidi kukithiri. Ufa kati ya matajiri na maskini wa Bongo inazidi kuongezeka. Rasilimali zetu zinazidi kuporwa. Na nchi imeingia gizani kama ilivyotabiriwa na wadau wa umeme.

Sasa nimeamua kurudi kubeba maboksi. Natumai nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Kama nitapata jibu, basi labda nitajipanga upya na kurudi tena kujiunga na wanaharakati kujaribu kuendeleza taifa hili. Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.

*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?
 
Harakati sasa basi, narudi beba maboksi
Serikali ya ukwasi, mbona yapigwa pasi
Umaskini wa Masasi, watanda kwa kasi
Hata yetu mabasi, nayo yana ukakasi

Ufisadi uso kiasi, umetandawaa kwa kasi
Chama Cha Makwasi, chakaa na papasi
Mapapa kwa visasi, watetana kwa asasi
Ya'nini kubaki basi, ilihali twalinda maasi
 
Mwanaharakati hatoki
katikati ya mikakati
 
COMPANERO shujaa haogopi kuuwawa ,fight for your own right ,je kama wewe utakimbia ,kabuche akimbie ,Mwanakjj nae akimbie na wote tuamue kukimbia what is next ?? nini hatima ya nchii hii inayoelea katikati ya bahari pasipo kuwa na msaada wowote
kaza buti ni jukumu lako kukomboa nchi yako
 
mkuu unaweza kuacha harakati za mojakwamoja na ukaendelea naharakati chini kwa chini huko utakakokuwa,ni wengi sana wapo nje ya nchi lakini mchango wao kwenye harakati za ujenzi wa nchi yetu unafahamika,na wewe unawajua,nakushauri jiunge na hao mkuu
 
To retreat is not to surrender said Bob!
 
kabebe boksi mkuu!tuachie bongo yetu wazawa
 
 
Acheni idealism. Kuweni realistic.
 
 

Tanzania yenye neema bila mdhaifu na mwoga companero inawezekana. Kabebe maboksi mkuu, tuachie nchi yetu watanganyika.
 
 
...nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania...
Kauli hiyo ndio inanifanya nikupe b uendelee na mipango yako. Kwanza nani alisema kuwa wabeba maboksi hawana mchango katika harakati? naamini hata huko utakakoenda, utaendelea libeneke
 
 
Kukimbia tatizo sio suluhisho..dawa ni kukabili tatizo
 
Campanero,UANAHARAKATI sio nguvu ya soda!! Sisi wengine tumeamua kuwa ingawa tunalipata joto la jiwe tutapambana na hawa mafisadi mpaka lyamba!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…