Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hapa nchini inazidi kuwa tete, hii ikiwa ni miaka 5 toka nirejee kwa moyo wote kuja kujenga Taifa. Pamoja na harakati zote hizo bado hali ya umaskini inadhidi kukithiri. Ufa kati ya matajiri na maskini wa Bongo inazidi kuongezeka. Rasilimali zetu zinazidi kuporwa. Na nchi imeingia gizani kama ilivyotabiriwa na wadau wa umeme.
Sasa nimeamua kurudi kubeba maboksi. Natumai nitatumia muda huo kutafakari ni wapi nilikosea katika harakati zangu za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Kama nitapata jibu, basi labda nitajipanga upya na kurudi tena kujiunga na wanaharakati kujaribu kuendeleza taifa hili. Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.
*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?