Hatuendi popote mpaka kieleweke hapa hapa Bongoland!
Kilimo kwanza kilimo, huo usanii ganiJamani pesa ile ya EPA, sasa yarudi kwa Jitu Mtapeli,
Chunguza sakata la richmond, kumbe mkulu faili liko mezani,
wabunge waamua kuvimba, Mkulu nayeye kazimika,
Companero badilisha mawazo, nenda kwenye kilimo kwanza.
Ndugu yangu mafanikio yepi? Kwenye maboksi watu wanazamia hata kwa kutambaa. Tena wanajilipua. Wengine wanacheza bahati nasibu ya Kijani!kwani huko kwenye maboksi mnaendaje? maana wenzetu mna kisimati kweli, umeme umekatika viyoyozi ndani havifanyi kazi mmechoka kujipepea na magazeti haaoo mnapanda pipa kwenda kwenye maboksi...winter ikianza mkimiss fukuto la bongo haaooo mnapanda pipa mnarudi...Companiero tafadhali weka bayana siri ya mafanikio yako
Home depot ziko nyingi, hiyo iko wapi - South Central LA au pale Inglewood?
Sawa sawa, aidha kwa upande wako licha ya kutoweka wazi namna ulivyoendesha harakati zako na namna ulivyoshindwa, unakaribishwa tena kubeba maboksi....
Hiari yashinda utumwa
Pole sana mkuu! Nchi c yetu tena hii... Wachache ndyo wanaitafuna...Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.
*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?
Mkuu,
Harakati zako za ukombozi wa nchi ulikuwa unazifanyia wapi na kwa staili gani? Labda ungetudokeza vilevile, ulijihusisha na kitu gani katika harakati hizo na mikakati uliyotumia.Pengine kwa kufanya hivyo wanaJF wataweza kukuonesha sababu za kutofanikiwa kwa jitihada zako. Yamkini ulielekeza nguvu kusiko, ama kama kaa la moto; ulitaka uwake mwenyewe bila ushirikiano na makaa wenzako.
Kwenye mapambano ni mwiko kuelezea mbinu zako. Adui aweza kusikia. Na ikawa balaa. Kumbuka historia ya ENIGMA!
Yanabebwa huko alipo Julius. Kashatoa dokezo. Ila kuna shughuli nyepesi zaidi za unesi.
Companero:
Nilishaanza kujitoa ushiriki wangu hapa JF. Lakini kwa sababu wewe ni mtani wa jadi nimehamua kurudi kwa posti hii.
Kutokana na utangulizi wa posti yako, najihisi kama NABII VILE. Miaka 5 iliyopita ulinipa ushauri wa kurudi, na sababu zilizonifanya kukataa kurudi ni zile unazoziona sasa.
Anyway mimi naanza ukabaila huko, naomba mvua ziwe nzuri tu mwaka huu.
Kufichaficha mbinu matokeo yake yaweza kuwa mazuri au mabaya, mojawapo ya mabaya ni kukosa ushirikiano na wana mapambano wenzako