Harakati Sasa Basi - Narudi Kubeba Maboksi!

Harakati Sasa Basi - Narudi Kubeba Maboksi!

Jamani pesa ile ya EPA, sasa yarudi kwa Jitu Mtapeli,
Chunguza sakata la richmond, kumbe mkulu faili liko mezani,
wabunge waamua kuvimba, Mkulu nayeye kazimika,
Companero badilisha mawazo, nenda kwenye kilimo kwanza.
 
Mkuu Comp! Kwani wewe elimu yako iko vp? kwa nini ukabebe mabox hamna white colar job huko??
 
Hatuendi popote mpaka kieleweke hapa hapa Bongoland!

Join Date: Mon Feb 2006
Location: UK
Posts: 3,064
Thanks: 682
Thanked 1,323 Times in 778 Posts
Rep Power: 29

kwi kwi kwi ...lol
 
kwani huko kwenye maboksi mnaendaje? maana wenzetu mna kisimati kweli, umeme umekatika viyoyozi ndani havifanyi kazi mmechoka kujipepea na magazeti haaoo mnapanda pipa kwenda kwenye maboksi...winter ikianza mkimiss fukuto la bongo haaooo mnapanda pipa mnarudi...Companiero tafadhali weka bayana siri ya mafanikio yako
 
Jamani pesa ile ya EPA, sasa yarudi kwa Jitu Mtapeli,
Chunguza sakata la richmond, kumbe mkulu faili liko mezani,
wabunge waamua kuvimba, Mkulu nayeye kazimika,
Companero badilisha mawazo, nenda kwenye kilimo kwanza.
Kilimo kwanza kilimo, huo usanii gani
Uti wa mgongo, siyo Kilimo asilani
Uchumi wa Bongo, sasa ni madini
Wajinga ndo waliwao, ni si maskini
Sikiliza Ticha lao, nalo lo likighani:

Kuwasomesha watoto
Imekuwa adha nzito,
Mambo mengi hatuwezi,
Tumeachia wazazi

Vitabu na madawati
Hupata wenye bahati,
Wasopata wadhamini
Huchora, huketi chini

Waumwao ni taabu
Kupatiwa matibabu
Sana wengi hawajali,
Hawendi hosipitali

Kupunga matumizi
Twakata wafanyakazi
Na wale wanobakia
Kuwalipa ni udhia

Balozi za ugenini
Zinaishi kwa madeni
Imekuwa ni taabu,
Acha soni na aibu

Viwanda tunatangaza
Kutafuta kuviuza,
Tukikosa wanunuzi
Kuvyendesha hatuwezi

Wakulima twawakopa.
Tunashindwa kuwalipa,
Pembejeo hatuwapi,
Hatujui tupatepi

- Nyerere, 1993, Tanzania! Tanzania!
 
It's about time you stop wallowing in utopian fantasy and get back to reality.

Njoo hapa....Home Depot is hiring...
 
kwani huko kwenye maboksi mnaendaje? maana wenzetu mna kisimati kweli, umeme umekatika viyoyozi ndani havifanyi kazi mmechoka kujipepea na magazeti haaoo mnapanda pipa kwenda kwenye maboksi...winter ikianza mkimiss fukuto la bongo haaooo mnapanda pipa mnarudi...Companiero tafadhali weka bayana siri ya mafanikio yako
Ndugu yangu mafanikio yepi? Kwenye maboksi watu wanazamia hata kwa kutambaa. Tena wanajilipua. Wengine wanacheza bahati nasibu ya Kijani!
 
It's about time you stop wallowing in utopian fantasy and get back to reality.

Njoo hapa....Home Depot is hiring...

Home depot ziko nyingi, hiyo iko wapi - South Central LA au pale Inglewood?
 
Mkuu,
Harakati zako za ukombozi wa nchi ulikuwa unazifanyia wapi na kwa staili gani? Labda ungetudokeza vilevile, ulijihusisha na kitu gani katika harakati hizo na mikakati uliyotumia.Pengine kwa kufanya hivyo wanaJF wataweza kukuonesha sababu za kutofanikiwa kwa jitihada zako. Yamkini ulielekeza nguvu kusiko, ama kama kaa la moto; ulitaka uwake mwenyewe bila ushirikiano na makaa wenzako.

Laiti kama kurejea kwako katika maeneo ya kubeba maboksi kutaweka kipaumbele katika kutafuta elimu (kama silaha) utakayorejea nayo siku moja kuendeleza harakati.
By the way dokezo la mabox yanakobebwa litasaidia wengi, pengine hata mimi.
 
Sawa sawa, aidha kwa upande wako licha ya kutoweka wazi namna ulivyoendesha harakati zako na namna ulivyoshindwa, unakaribishwa tena kubeba maboksi....

Hiari yashinda utumwa

Hawa mafisadi wa CCM wanafurahi wakisikia mmoja katika wapambanaji amepungua; lakini walivyo na akili finyu hawaelewi kuwa comrade hajatupa taulo kwenye ulingo bali anabadilisha uwanja wa mapambano . Siku hizi teknolojia inaturuhusu kupambana na mafisadi hata kwa masafa marefu!!
Comrade is just relocating kama vile wakina Samora walivyokuwa Bongo wakati wakipigana na wareno Msumbiji.
 
Mkuu Comp! Kwani wewe elimu yako iko vp? kwa nini ukabebe mabox hamna white colar job huko??

Ni elimu ya scribbling, wapi kuna dili hilo huko maana zile dalley na 'I got it' za maboksi noma!
 
Kwa sasa roho inataka ila mwili ni dhaifu. Naam, nia ya kubaki na kuvumilia ninayo, sababu ya kubaki na kuvumilia ninayo, ila uwezo wa kubaki na kuvumilia sina.

*Wapi maboksi yanabebeka kwa tija na elimu nzuri ya maendeleo inapatikana?
Pole sana mkuu! Nchi c yetu tena hii... Wachache ndyo wanaitafuna...
 
Mkuu,
Harakati zako za ukombozi wa nchi ulikuwa unazifanyia wapi na kwa staili gani? Labda ungetudokeza vilevile, ulijihusisha na kitu gani katika harakati hizo na mikakati uliyotumia.Pengine kwa kufanya hivyo wanaJF wataweza kukuonesha sababu za kutofanikiwa kwa jitihada zako. Yamkini ulielekeza nguvu kusiko, ama kama kaa la moto; ulitaka uwake mwenyewe bila ushirikiano na makaa wenzako.

Kwenye mapambano ni mwiko kuelezea mbinu zako. Adui aweza kusikia. Na ikawa balaa. Kumbuka historia ya ENIGMA!
 
Companero:

Nilishaanza kujitoa ushiriki wangu hapa JF. Lakini kwa sababu wewe ni mtani wa jadi nimehamua kurudi kwa posti hii.

Kutokana na utangulizi wa posti yako, najihisi kama NABII VILE. Miaka 5 iliyopita ulinipa ushauri wa kurudi, na sababu zilizonifanya kukataa kurudi ni zile unazoziona sasa.

Anyway mimi naanza ukabaila huko, naomba mvua ziwe nzuri tu mwaka huu.
 
By the way dokezo la mabox yanakobebwa litasaidia wengi, pengine hata mimi.

Yanabebwa huko alipo Julius. Kashatoa dokezo. Ila kuna shughuli nyepesi zaidi za unesi.
 
Kwenye mapambano ni mwiko kuelezea mbinu zako. Adui aweza kusikia. Na ikawa balaa. Kumbuka historia ya ENIGMA!

Kufichaficha mbinu matokeo yake yaweza kuwa mazuri au mabaya, mojawapo ya mabaya ni kukosa ushirikiano na wana mapambano wenzako
 
Companero:

Nilishaanza kujitoa ushiriki wangu hapa JF. Lakini kwa sababu wewe ni mtani wa jadi nimehamua kurudi kwa posti hii.

Kutokana na utangulizi wa posti yako, najihisi kama NABII VILE. Miaka 5 iliyopita ulinipa ushauri wa kurudi, na sababu zilizonifanya kukataa kurudi ni zile unazoziona sasa.

Anyway mimi naanza ukabaila huko, naomba mvua ziwe nzuri tu mwaka huu.

Modeli za maendeleo za Tanzania ni 'evolutionary' na sio 'revolutionary'. Na kwa kawaida michakato ya ki-evolutionary inachukua karne kadhaa kuleta mabadiliko. Tunahitaji watu kama kina Hugo Chavez kuleta 'revolutionary' change!
 
Kufichaficha mbinu matokeo yake yaweza kuwa mazuri au mabaya, mojawapo ya mabaya ni kukosa ushirikiano na wana mapambano wenzako

Wapambanaji wa kweli tunajuana kwa vilemba. Tunashirikiana na kupeana mbinu kwa siri. Hatumwagi mtama kwenye kuku wengi - wa kienyeji na kisasa!
 
Back
Top Bottom