babu we kuna watu wanazo in excess na kuna ambao hawana,hili likiranga lilivyo selfish linaona starehe iwe kwa walionazo tu!hovyo sana...
ni hivi waache wenye nazo na hawamind kushare kile walichonacho wafanye wanavyopenda! wewe kama unazo na hutaki kutoa kwa wasio nacho then kimpango wako!....dada charity is nobody compare to 60,000 people ambao wako expected to turn up kwenye hio match!......hata usipompa ticket akawa mmoja wao,still kuna significant amount of people will turn up...huoni kama UNALEKEZA MAGUVU YAKO MAHALI SIPO?!!!
dada charity pia hajasababisha uhaba wa madawati na ukosefu wa vitanda mahospitalini....MAHASIRA YENU pelekeni huko huko mlikoyatoa wacheni kumfanya scape goat....
afu wee kiranga kama wewe ni smart sana mbona hausikiki kny vitabu kama akina galileo na isack newton???this topic was meant to be a joke...kama hukuona hilo una walakini....and dont drag us into your shit hole of madness!:angry:
Wewe ni mgumu sana wa kuelewa.
Ni hivi, mimi sina tatizo na wenye nazo kutumia wanavyotaka. Naamini katika uhuru wa matumizi.
Nisichotaka ni pale wasio nazo nao wajidai kutaka kuishi maisha ya kifahari kama wanazo. Sitaki tamaa ya watu kutaka kuishi maisha wasiyoyamudu, kesho keshokutwa watakuja kuweka rehani mpaka pete za ndoa ili kwenda kuendekeza anasa za mpito. Watakula ada za watoto ili kuendekeza anasa za mpito. Watatumia kodi ya nyumba kuendekeza anasa za mpito. Wataiba kazini kama alivyosema mkuu mbebabox hapo juu, ili kuendekeza anasa za mpito.
Heck, watasaliti hata unyumba ili kuendekeza anasa za mpito, what is to stop them from getting the next high?
Tatizo si ku share, mbona ku share tuna share sana, kutoa tunatoa sana tu, fuatilia post zangu nyuma uone.
Tatizo unatoa kwa kitu gani? Si kila kutoa kuzuri.Teja la madawa ya kulevya likija kukuomba ili lijidunge utatoa? Kwa sababu kutoa ni vizuri?
Una finance habit ambayo ni mbaya kama drug addiction kama utampa huyu Charity pesa ili aende kuangalia mpira, mpira wa gharama za ajabu kwa mtu asiye na hela, mpira ambao ukiuangalia sana unalitia taifa hasara tu.
Mimi naongelea principles zinazosimama kama first principles, you don't get something out of nothing.Usijaribu kabisa maisha haya kujifanya unajua kudandia migongoni mwa watu, utakuta umedandiwa wewe.
Ukimtetea sana naweza kupata fikra kwamba vinakuuma kwa sababu na wewe ni wale wale wa kutegeshea na kusubiria vibopa vijipigepige, maisha ya unyonge na utegemezi yataisha lini haya?
Ndiyo nyie kinamama mnaodai usawa na wanaume? WaBeijing nyie? Anything you can do I can do better nyie/
Usawa mtaupata kwa kuwa tegemezi kama hivi? Hivi mtu ombaomba anaweza kujisikia na yeye akasema na mimi nina sauti mbele ya wafadhili wake?
Kati yangu mie ninaetaka kumpa huyu dada tough love ili ayaweke mambo yake sawa na hatimaye maisha yake yamwendee sawa in the long term, na nyie mnaotaka kumpa sumu ili awaone mnampenda nani selfish?
Kati yangu ninayemwambia ukweli utakaokuja kumuepusha na mabalaa kedekede, hasa kwa sababu hamna cha bure dunia hii na mwanamke ombaomba anajirahisisha na ni rahisi sana kupata mabalaa ya wanaume wakware, na nyie mnaomwambia kuomba ni poa tu, nani selfish?
Kati yake yeye Charity anayetaka kuwabebesha gharama zisizo lazima wenzake, ambao tayari tushaona wana michango na majukumu mengine kedekede tena ya muhimu zaidi, na mie ninayesema jamani ni lazima tufikirie kuhusu misaada tunayoomba ili iwe ya tija na tusiwakwaze wenzetu kwa kuomba misaada ya anasa zisizo tija, nani selfish?
Sio unaandika vitu bila kufikiri t, utaja jivua nguo mbele ya kadamnasi na kudhihirisha utupu wako wa fikra.