pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Walishinda mechi zao zote bila kufungwa bao hata moja kwenye CECAFA Women's Cup. Baada ya kuwagaragaza na kuwabingirisha bingirisha kama vikaragosi wenyeji wao Kilimanjaro Queens. Kabla ya hiyo walifika fainali za kufuzu kushiriki kwenye 2020 Tokyo Olympics. Leo Harambee Starlets wameendeleza utamaduni wao wa kushinda, nje ya bara hili, kule Golden City Sports Complex, Uturuki kwenye Turkish Women's Cup. Wameng'aa kweli kweli kwenye mechi yao ya kwanza, baada ya kuilaza N.Ireland 2-0. Hongera kwa kina dada zetu, na wazidi kuiwakilisha Afrika Mashariki Kenyan style bila kusita sita. Make us proud ladies and make them go green with envy. [emoji1139][emoji1139][emoji1139]