Harambee Stars(Kenya) wapo Ufaransa , The Cranes(Uganda) wapo Abu Dhabi, Les Léopards(DRC) wapo Hispania. Je, Taifa Stars(Tanzania) wapo wapi?

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Posts
24,386
Reaction score
57,588
Mimi napenda sana football napenda kuona mataifa mbalimbali yanapozipa kipaumbele team zao na hata kuzigharamia kwenda mataifa ya nje kujifua ili kujiandaa na AFCON. Nasikitika sioni kabisa amsha amsha kwa team yetu ya Taifa stars.

Kwanza hivi zile million kumi kumi zao walishapewa?

Tanzania tunajiandaa vipi kwenda kushiriki AFCON? Naona kina Samatta wanaendelea kuhudhulia iftar tu huku kina Okwi wapo Abu Dhabi wakijifua.

Tukifungwa Hamsa au Hamsa mbili tutamlaumu wachezaji, kocha. Je tumewapa chances za kujiandaa?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars.
 
Wapo Malawi kwa rafiki yake JIWE....

Huko kwa mabeberu hawawezi kwenda.
 
Kama kagera ilishuka daraja halafu ikapanda muda huo huo huo unategemea nini kutoka tff taasisi ya kusimamia maendeleo ya mpira Tanzania , ligi ya mwaka huu imekuwa mbovu kuliko ligi zote zahera akisema anashambuliwa. Hawa jamaa wa tff hawana malengo kabisa watasema lengo lao ilikuwa kufuzu misri , sasa hivi wana resti
 
Kazi na lengo kuu la Tff ni kuhakikisha Simba anakuwa bingwa. Na kuwamaliza maadui wa simba kama vile Kagera S.
 
Kila siku nasema mkuu watu hawnielewi narudia tena sisi tumelogwa na alie tuloga kafa maana hatujielewi na hatujui kinacho kuja mbele ni nini.tupotupo.tukienda huko tukapigwa kumi ndio watu wataekewa. Sasa hivi TFF wamelala kabisa kama vile hatuendi again. Naomba muendelee kulala hivyohivyo shenzi Taipu
 
Hii chuki kwa Mh. Rais itakuisha lini mkuu.

Maana unachuki kupitiliza as if Mkuu amemchukua Mama Jesca kutoka kwako.
Kuna wengine tuna chuki naye hadi tumeshindwa kuiweka hadharani.

Haki huleta upendo na amani bali dhuluma na uonevu huleta chuki na visasi hutawala.

Watu wamelazimishwa kutulia ila amani imetoweka mioyoni mwao
 
Sisi Tz tunasubiri bonanza la Samata na kiba lipite kwanza.
 
Ubovu wa ligi kuliko miaka yote upo wapi...yanga wasipochukua ubingwa basi ligi inageuka kuwa mbovu...haya mbona hamkuyasema kipindi mnachukua ubingwa mara tatu mfululizo...nyie tulieni dawa iwaingie vizuri hakuna namna
 
Ungekuwa kocha wa Taifa Stars baada ya kusikia Harambee Stars wapo Ufaransa ungekurupuka kupeleka timu Belgium, Spain nk. Akili za kuiga
 

Huenda TFF wanadhani TZ itapewa mechi za viporo huko Misri
 
Huenda TFF wanadhani TZ itapewa mechi za viporo huko Misri
Hapana bwana,labda wanaona hawatatoboa hata wakijiandaa.Ila donner kantri tunashindwa fanya maandalizi kwa team yetu kweli ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…