Salama wakuu
Mwaka 2018 niliuza laptop niliyotumia miaka mitano ilikuwa na hard disk gb 500, kabla sijaiuza nilikuwa nimeshanunua laptop nyingine yenye hard disk TB 1, nilichofanya nilihamisha vitu vyote vya hard disk ya zamani kwenda hard disk ya computer mpya.
Hadi sasa hio hard disk ya TB 1 naitumia hadi sasa kwenye laptop na ni karibia kila siku, Laptop niliwahi kubadili mwaka 2020 lakini hard disk niliweka ile ile ya tagu 2018 nayotumia mpaka sasa,
Nimeona niulize kama pana usalama wa kuendelea kuitumia maana ni mwaka wa 5 huu.