Harmonize aandika jina la Mama yake range rover anayoimiliki

Harmonize aandika jina la Mama yake range rover anayoimiliki

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Tunaweza kusema kuwa Harmonize ni moja kati ya wasanii wanaomuenzi mchezaji machachari wa PSG Achraf Hakimi kwenye harakati za kukwepa kuibiwa mali na Wanawake wa mjini.

Range Rover ya Msanii Harmonize kwenye Registration number jina linasoma Habiba Chivalavala, hilo jina sio la mtu mwengine isipokuwa ni jina la Mama yake mzazi msanii Harmonize.

Namba za Gari ni T 790 EBX.
20240213_221116.jpg


Harmonize ni moja kati ya wasanii wenye mafanikio makubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Nmekumbuka ila kauli ya wazazi masikini kwa watoto wao kuwa urithi wao ni elimu na sio nyumba wala mali yoyote halafu hapo unakuta mzazi mwenyewe hana mali yoyote anayomiliki.

Anyway, bc tuseme sawa
 
Kiherehere kingine bwana.

Sasa, tukuamini wewe mwenye taarifa za Habiba au tuuamini Mfumo ulioutumia kwa kuingiza namba za Gari la Habiba asiejulikana.

Mfumo unasema gari nyeupe,
Gari uliyotuwekea sio Jeupe, unaweza kufafanua huo mkorogo??
 
Hamna mafanikio yoyote ni maigizo tu! Msanii mwenye mafanikio akagombanie M5 club??

Tena hiyo million 5 yenyewe ya kupewa na mcheza kamali?
Wasanii Hawa msiwaone mitandaon wakijitamba ni choka mbaya vibaya sana Bora hata fundi ujenzi. Kuna mmoja maarufu tu alinikopa ten mpaka Leo hajanilipa
 
Back
Top Bottom