Habari wale wapenda buradani.Hope ni wazima...
Kwanza nampongeza kijana mwenzangu hormonize kwa kuanzisha familia yake mpya(konde gang).Hii ni hatua nzuri ya kukua na kuelekea kwenye kutengeneza himaya yako siku za usoni.
Mara nyingi sana nimekuwa nikitofautiana na baadhi ya watu wanaobeza hatua ya harmonize kujitoa wasafi na kuanzisha familia yake.Lazima tumpongeze kwani inapelekea kukua kwa tasnia ya muziki kwa hapa Tanzania.
Nadhani Harmonize alijuwa ule msemo usemao"You will never be a rich by working in someone else"
Watu wote waliofanikiwa hawafanyi kazi chini ya mtu,kwani kitendo cha kuwa chini yake kinakufanya uwe na mipaka ya kiutendaji hivyo hauwezi kuwa juu ya boss wako.
Ngoja niingie kwenye mada.Harmonize acha kutafuta public sympathy.
Baada ya Harmonize kuanza kuonyesha dalili mbalimbali za kutaka kujitoa wasafi,Kuna mengi sana ambayo wapenzi na mashabiki wa wasafi waliyasema hasa zaidi ni lengo la Kuacha kum support Katika kazi zake za muziki.
Nadhani hili Harmonize alilijuwa mapema hivyo alijiandaa namna ya kulikabili.
Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Harmonize amejitoa kwa diamond na wasafi chuki ilizidi kuongezeka kwa mashabiki wa wasafi,na kweli walianza kususia kazi zake ushahidi ni huu wimbo alioutoa wiki hii (Eddy kenzo x Harmonize).
Harmonize lazima ajuwe kitendo Cha yeye kujitoa Katika familia yake iliyomlea kwa muda mrefu ametanga vita na wanafamilia yake hiyo (wasanii+blood fans).Hivyo aache kujipendekeza na kutafuta huruma ya watu.
Kitendo Cha ku-support na kutangaza kazi za wasafi so vibaya lakini lazima atambue kuwa wale ni maadui zake Sasa..
Si kitendo kibaya kibinadamu hasa kwa watu ambao wameshirikiana Mambo mengi lakini ki strategy ni kosa kubwa Sana na litamgharimu pakubwa.Hakuna asiyejuwa kuwa~
Harmonize ni mtunzi mzuri wa mashairi hivyo naamini ni msomaji mzuri wa vitabu.
Kama hajasoma kitabu # The art of war cha Sun Tzu.
Namuomba akitafute na akisome kitamsaidia sana Katika safari yake hii mpya aliyoainza.Namhakikishia hii ni safari yake ngumu na nzito kuwahi kusafiri.
Haya ni masomo matatu(3) ambayo Harmonize anaweza kuyapata Katika kitabu cha The art of war
#Lesson 01. Every battle is won before it is Fought.
(Know your strength and your enemies weakness and start preparing)
Vita yoyote ile inaanza kupiganwa kimkakati kwanza kabla ya kuenda kwenye open ground (war field).Hapa kila upande unaanza kwa kujiandaa na kukagua silaha zako vizuri kabla ya kuanza kushambulia.
Hapa lazima ujue nguvu zako na mapungufu ya adui yako ili upige sehemu sahihi.
Licha ya Harmonize kuishi Katika familia ya wasafi kwa muda mrefu lakini ameshindwa kutambua madhaifu na nguvu ya wapinzani wake(wasafi-daimond).Kitendo cha kuonyesha bado anajali alipotoka anakiuka somo namba moja Katika kitabu cha The art of war.
Hii itamgharimu sana kwani wenzake hawana huruma naye hata kidogo.
#Lesson 02.Before engaging, prepare to pay the price
(The only way to achieve Greatness is willingness to put it all in the line)
Kabla kuanzisha vita/mabishano lazima ujiandae kulipa gharama.
Mwanzo kabisa wakati nasikia habari za Harmonize kujitoa wasafi nilijuwa kuwa lazima atakuwa amejipanga na kujiandaa kwa figisu figisu kutoka Katika familia yake hiyo.
Ameishi na Sallam,mkubwa fella,Babu Tale pamoja na Diamond kwa muda mrefu hivyo anajuwa mbivu na mbichi zao.
Hivyo kitendo cha kujitoa alipaswa ajuwe kuwa litamgharimu sana lakini hakujiandaa kwa hili.
Hapa naweza kusema kuwa harmonize hakujiandaa ila alikurupuka.
#Lesson 03.Remain flexible in your Approach but not your results.
(Situation will change, you must adapt and keep pushing forward)
Hili ni funzo muhimu sana kwa Harmonize ili kuendelea vizuri na keria yake ya muziki.
Hii mbinu yake ya kujipendekeza kwa wasafi-daimond na kutafuta huruma kwa jamii haitamsaidia bali itaangukia pua.
Wapinzani wake washajuwa tayari kuwa Harmonize anatapa tapa na kuomba msaada wa ku push kazi zake indirectly hivyo watajiandaa kumkabili kirahisi sana.
Mbinu ya kujipendekeza haifai kwa sasa kwani wenzake hawata fanya hivyo,hawata muonea huruma bali watamkabili vilivyo.
Hapa ngoja niseme ukweli diamond atatumia kila mbinu ili kumuangusha Harmonize ili liwe funzo kwa wale waliobaki.
Naomba Harmonize atafute hiki kitabu naamini kitamsaidia Katika safari yake hii ngumu ya kimziki.
NOTE: Mashabiki kindaki ndaki wa Diamond na wasafi najuwa hawatapenda nilichokifanya hapa kwa kumkumbusha Harmonize.Naomba tuvumiliane.