Msanii anayetamba katika soko la Afrika Mashariki anayefahamikwa kwa jina la Harmonize, amehimiza wananchi wafanye maombi kwa Nigeria kutokana na machafuko yanayoendelea hivi sasa. Harmonize ametumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba watu wote kuiombea Nigeria.
===
Hatua hiyo imeonekana kuungwa mkono na msanii chipukizi Ibraah aliyechini ya label ya KondeGang
Labda wametarget soko la niajeria ila wanachofanya hawa wasanii kufumbia upuuzi wa nchi kwetu na kutoa mimacho kwa upuuzi huo huo unaofanyika nchi nyingine nawaona kama WAJINGA na MIMBURULA.
Nchini kwenu mnapalilia machafuko majukwaani kwa kuwaita Watanzania wenzenu "Misukule" kisa wako vyama tofauti na chenu, Leo mnajifanya mna uchungu na Nigeria kuliko Tanzania? Au huyo Hamonaizi ni Mmsumbiji?
Lowassa 2015 pamoja na udhaifu wake lakini alipoimba Elimu Elimu Elimu Elimu alikua sahihi sana...kuna muda ukiwasikiliza vijana aina ya hawa wasanii unaweza shikwa na hasira ukaua mtu ni wamejaa upumbavu tu kichwani kwao wapo tayari kuchekelea hata mauaji kwa wenzao ili mradi wao mkono uende kinywani pumbavu.