Harmonize Alishea Penzi Na Paula Kabla Ya Kajala Masanja, Kitaalamu Imekaaje

Harmonize Alishea Penzi Na Paula Kabla Ya Kajala Masanja, Kitaalamu Imekaaje

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Sakata la kale limeibuka upya na kuchafua mitandao ya kijamii nchini kufuatia madai mazito kwamba staa wa Bongo Fleva, Harmonize, alianza uhusiano wa kimapenzi na Paula kabla ya kuhamia na kufanya mapenzi na mama yake, Kajala Masanja. Zogo hili jipya limezuka baada ya video ya mahojiano ya kipindi cha A-List kusambaa kwa kasi, ikimwonyesha muigizaji Irene Uwoya akimlipua laivu Kajala kwa kumwambia kuwa yeye ndiye aliyemnyang'anya binti yake mwanamume na kuingilia penzi lao wakati mtoto huyo akiwa bado yuko in love.

Akiitikia madai hayo kwa mshtuko mkubwa, Kajala Masanja amekiri kuwa suala hilo limekuwa likimuumiza kichwa kwani hadi leo hajui ukweli mzizi wa nini kilitokea kati ya Paula na Harmonize . Kajala alifunguka kuwa kila akijaribu kumuuliza Paula ukweli wa jambo hilo amekuwa hapewi jibu lililonyooka, hali inayozidi kuacha maswali mengi miongoni mwa mashabiki wanaokumbuka skendo ya mwaka 2021 ambapo Harmonize alidaiwa kumtumia Paula picha za utupu.

Wakati huohuo, wadau wakubwa wa burudani wakiongozwa na Mwijaku wamemjia juu Kajala kwa kuruhusu mahojiano hayo kuruka, wakidai ni kutafuta kiki (clout chasing) kunakomdhalilisha Paula ambaye kwa sasa ametulia kwenye ndoa yake na msanii Marioo. Mashabiki wengi mtandaoni wamelaani kitendo cha kufukua makaburi hayo ya kale, wakisisitiza kuwa kinaweza kuvuruga amani ya familia ya Paula na Marioo ambao tayari wana mtoto wa pamoja.
 
Sasa huyo Kajala anaongea nini hiko mbona haeleweki....
Kama anakuja halafu anapotea...😁😁wangetulia tuu wazeeke kwa amani kuliko kuforce mambo na kuaibikia ukubwani
 
Wote Malaya tu hapa

Huyo wolper kaliwa na Ali kiba kaliwa na jux kaliwa na diamond kaliwa na harmonize hebu tazama hiyo circle Kwanza

Wakati wolper analiwa na Ali kiba at the same time Alikiba ana mla Lulu Elizabeth Michael

So hao kushare mabwana kwao sio story
 
Back
Top Bottom