Kuna wakati wasanii huwa wanapata pressure sana kiasi kwamba, huwezi kujua wanaimba nini aisee.
Unakuta msanii kachoka, hana mood lakini analazimisha tu kufanya kazi.
Hata huyu Harmonize naona anajitahidi, hali hii iliwahi kumkuta pia Diamond wakati akiwa na pressure za Kiba na Clouds.
Kuna mshkaji wangu fulani ni Shabiki lialia wa Diamond tangu enzi hizo ana mdomo mkubwa, akawa anasema jamaa anapata kollabo kubwa ajitahidi basi kuimba vizuri. Kwa maoni yake anasema jamaa alikuwa anaimba vibaya halafu, video anakimbia kimbia tu ( wakati huo ametoa video ya Nana feat Mr. Flavor)
1- Kwenye wimbo alioshirikishwa na Waje unaitwa Coco baby, yaani alipuyanga kiwango cha 4G.
2- Wimbo wake wa Kidogo feat Psquare, binafsi huwa naona Peter ndio kaimba fresh. Diamond alikuwa anapumua pumua tu yaani.
3- Diamond feat Mafikizolo, kile kisauti sijui alikitoa wapi maana sijawahi kumsikia akikitumia tena kwenye wimbo mwingine.
Kwahiyo nadhani huwa ni suala la muda tu.