Harmonize ana mpango wa kufanya collabo na Ali Kiba na pia amsifia

Harmonize ana mpango wa kufanya collabo na Ali Kiba na pia amsifia

Mtanzania Mkenya

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
238
Reaction score
387
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds FM Ijumaa hii,
Harmonize aliulizwa kama anaweza kufanya kazi na Ali Kiba
kama ikitokea nafasi.

“Unajua Ali Kiba ni msanii wa Kitanzania, ni msanii mzuri pia,
so kolabo ikiwa na tija nitafanya naye kwanini nisifanye naye.
Sio Ali Kiba tu, msanii yeyote wa Kitanzania,” alisema
Harmozine.

Mashabiki muache kuchonganisha jaman.
 
Kwani kuna tatizo au ugomvi wowote? mpaka wewe mleta post kikakufanya ulete UPASHKUNA?
 
Kwani kuna tatizo au ugomvi wowote? mpaka wewe mleta post kikakufanya ulete UPASHKUNA?


Tatizo mashabiki wanapenda kuchonganisha sana hizi pande mbili ilhali wasanii wenyewe hawana tatizo lolote baina yao.
 
Shida IPO wapi hapo!!
Ulitaka akatae
Kwani kiba ,au diamond kuna alie sema waziwazi hawezi Fanya korabo NA mwenzie!!?
Nyie ndio mnayakuza
 
Alisema atafanya kazi na kiba kama kutakuwa na mantiki sio kufanya ilimradi tu.
 
huyo dogo atakua anatafuta soko la kariakoo tu
Huyu dogo ni kajipu kadogo. Kama keshafanya kollabo na simba...alitakiwa levels za juu...kama kina AKA..Davido...2face aache watu Wa local
 
Back
Top Bottom