Harmonize, asante kijana umemuimbia mzee wetu kwa hisia

Harmonize, asante kijana umemuimbia mzee wetu kwa hisia

Msechu amekosa tu kundi la kumuunga mkono ila wimbo wake hauna mpinzani katika nyimbo zote zilizoimbwa juu ya hayati BEN MKAPA

Mwimbo huo ana cover, ameshawaimbia wengine waliofariki kabla. Anabadili names tu.
 
Wimbo bora wa kusikiliza ni ule wa chibonge PETER MSECHU wa Tutaonana MKAPA, ameutendea haki kila idara.
Hakika mkuu, na nilipanga kuja na uzi wa kumpongeza Peter msechu kwa wimbo ule wenye hisia kali na sauti ya kuvutia. Hakika PETER MSECHU kamtendea haki Hayati Mkapa .
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kwangu Nalia ya Ferooz na Roma naona ipo faya sana kwenye maswala ya misiba
Afu ifuatie ile Kifo ya Juma Nature
Ya Msechu ndo funga kazi...
 
Kawaida sana.
Hamfikii yeyote Waliosimama nyuma yake ,Ni waimbaji mahiri kopa,Misambano ..nk

Harmonize ni Maarufu si Mahiri.
Pengo kubwa sana kwa kuondoka kwa Komba,bado hajapatikana wa kuliziba.

R.I.P Mkapa.
 
Ile nyimbo ya msechu ilishaimbwa, kabadili mashairi tu Melody used. Ya konde boy Ni new song
Wewe unaweza kuwa umezaliwa siku za hivi karibuni. Huo wimbo wa kama sio juhudi zako kwanza uliimbwa na kwaya ya kijitonyama kkkt "Kama sio juhudi zako Yesu" ukafanyia marekebisho kipindi cha msiba wa nyerere "kama sio juhudi zako mwalimu" kwahiyo konde boy naye kaufanyia marekebisho
 
Hii nchi waigizaji hawako kwenye industry yao, walioko huko sio waigizaji
 
Nimesikiliza wimbo wa Harmonize, nyimbo ya maombolezo.

Kwa kweli asante sana kijana wetu, wimbo wako una hisia kali na umenitoa machozi. Kwenye wimbo Kijana kamlilia mzee, anasema kama siyo juhudi za mzee watu wa kusini lile daraja wangelipata wapi.

Kijana kaimba kwa hisia kali kwelikweli. Anaimba jinsi maraisi wenzie, Magufuli, Kikwete na Mwinyi wanavyomlilia.

Rest in Peace Benjamin Mkapa, You are our hero!

Mtafuta Kiki huyo
 
Samahani nje kidogo ya mada wakuu.
Naomba mwenye wimbo wa TUANUE MATANGA ulioimbwa na kapteni Komba zama zile za kumaliza msiba wa mzee Nyerere,mwenye nao saidia tafadhali.
 
Ule wimbo amecopy baadhi ya vitu ndio maana nyimbo zake zinaondolewa youtube nani hajui kipande cha wimbo wa Komba kuhusu Nyerere kama sio juhudi zako Nyerere Tanzania ingekuwa wapi
 
Marehemu Remmy Ongala (R.I.P) alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunga mashairi mara baada ya tukio. Rémy aliweza kutoa wimbo ndani ya masaa 24 baada ya tukio.

Kwahili Harmonize umenikumbusha mbali, kwakweli ulizaliwa kwasababu maalum.
 
Marehemu Remmy Ongala (R.I.P) alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunga mashairi mara baada ya tukio. Rémy aliweza kutoa wimbo ndani ya masaa 24 baada ya tukio.

Kwahili Harmonize umenikumbusha mbali, kwakweli ulizaliwa kwasababu maalum.
Acha kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Back
Top Bottom