Harmonize avunja record ya dunia ya kuachia Album inayosifia tu Mamlaka

Harmonize avunja record ya dunia ya kuachia Album inayosifia tu Mamlaka

Ni wazi kwamba hakujawahi kutokea msanii aliyewahi kuachia Albamu yenye nyimbo zinazosifia tu Mamlaka. Wasanii wengi uachia tu Single track za kusifia mamlaka au kiongozi wa juu wa serikali, lakini Mmakonde huyu ameenda mbali zaidi na kuachia Album yenye nyimbo zote zinazosifia Mamlaka na kiongozi wa juu wa serikali.

Uzinduzi wa Album hiyo uliuzuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Muheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Wageni wengine mashuhuri walioharikwa ni Diamond Platnumz, Rayvanny na Zuchu kutoka WCB ila hawakufika katika uzinduzi huo.

Mara nyingi Wasanii uitwa kioo cha jamii maana yake ni kwamba wanachoimba ndicho hutokea kwenye jamii. Kama atasifia mamlaka itamaanisha kuwa jamii nayo inalizishwa na mamlaka, na kama atapondea mamlaka itamaanisha kuwa jamii nayo haiko sawa na mamlaka.

Je alichokifanya Harmonize kutoa Albamu yenye nyimbo zote za kusifia Mamlaka ni sahihi kwa afya ya mashabiki na wasikilizaji wake ambao wana itikadi tofautitofauti za kisiasa?

Pia soma: Rais Samia ashiriki uzinduzi wa Album ya Harmonize Ukumbi wa Mlimani City, leo Mei 25, 2024
Anajiandaa kushiriki kampeni Mwaka huu na mwakani Bro. Yuko kimkakati zaidi
 
Hata kama ni CHUKI UNAYO siyo uandike UZULIWA ACHA ZAKO MKUU ACHA BHANA
 
Sio mbaya anatengeneza maisha ya wanawe na familia yake kwa ujumla,humu watu wengi wanabwabwaja sababu hyo nafasi hawajaipata.
 
Back
Top Bottom