Harmonize hajafanya ubaya

Kwa nini kuondoka Harmonize mnachukulia kama vita.Mimi mwenyewe nafurahi Harmo kujitegemea mwenyewe ,tatizo je amejipanga kwa fitina ?Usimwone Mondi ana shine jua nyuma ana watu wanampigania je yy anao?Kama anao ni kitu kizuri kama hana yy ndiye atakaye umia.Msimwone Belle 9 yupo kimya mkazani hana uwezo bali hana watu wakuupigania mziki wake.
Kuwa chini ya label ni kitu kizuri sana ,haswa kwa wenzetu US,Drake yule pamoja na kuwa na utajiri mkubwa,label yake ya OVO lakini bado yupo chini ya YCMB,we unazani kwa nini Drake hajaondoka YCMB label ya Lil Wyne na Birdman?

Kanye west ana label ya Good Life,ana brand ya Yeezy ambayo thamani yake ni zaidi ya USD 1 bilion,lakini pamoja na utajiri wake bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z,hujajiuliza kwa nini Kanye bado yupo chini ya Roc nation?

Rihanna sasa hivi networth yake USD 600m baada kama ya miaka mitatu au miwili atakuwa na USD 1bil ,lakini bado yupo chini ya Roc Nation ya Jay Z,wewe unazani kwanini Rihanna,Drake,Kanye West na hata Nick Minaj pamoja na utajiri wao lkn bado wapo chini ya label?

Label zina umuhimu wake sana sababu katika Industry hizi za Music kuna FITINA na KUBANIANA ,kwani kuna watu wakali lkn hawana watu wa kupush mziki wao.

Miaka ya nyuma kulikuwa na mwanamziki wa RnB Bob Valentino alivuma sana alipokuwa chini ya DTP Ludacris,baadaye akaondoka akamwambia Luda anataka kujitegemea,baada ya hapo Bob V akapotea mazima.
Vile vile kulikuwa na Rapper Chingy nae alikuwa DTP akazinguana na Luda,akwambia yeye anaondoka anataka kujitegemea Ludacris kamruhusu nae akapotea mazima
na nasikia hata Runtown wa Nigeria kapotea baada ya kuondoka kwenye Label.

Kuanzisha label au kujitegemea sio swala baya kwani hata yy anaweza wafungulia mlango wengine,lkn je amejipanga,mziki huu mgumu kwani umejaa fitina ,unahitaji watu wanaojua industry ili upush kazi zako.

Na ndio maana pamoja na kuwa na mihela yao wakina Rihanna,Kanye,Drake na Nick Minaj bado wapo chini ya Label.

Na Mziki wa Tz sasa hivi una hali mbaya yaani washikadau wamewagawa mashabiki,siku hizi team za kwenye mziki wetu,hazina utofauti na ushabiki wa Simba na Yanga,ili upate support unatakiwa uwe ndani ya hizi team,ukiwa nje umekwisha mfano tu Baraka da prince na Mavoko tushaanza kuwasahau.
 
Point kali sana
 
Mashabiki Wa harmonise cjui wafanye kumptishia huu ushauri.
Nakumbuka jeuri ya kijana anayepata balehe, akikasirika kidogo anasema naenda kujitegemea, wajifunze Kwa Yesu Kristo
 
Huko south Sudan hawaijuw wcb na amejaza kuliko mtuu yeyote Bongo ata wasafi festival haijawahi pata ... Yeye huwa haimbi nyegezi ao vumbi atatoboa tu
Kwan south Sudan walienda kumwangalia harmonize, hyo ilikuwa event ya kitaifa na ilikuwa free-entry...mpunga alipewa na serikali ya south Sudan, Nina mashaka na uwezo wa kondeboy kufight nje ya wcb, mziki wa tz una mambo mengi, fitina, ndumba, unafiki na kubaniana kwingi....
Mi naona afanye mipango yake, ajitanue awezavyo, apambane vya kutosha lakn asitoke nje ya WCB, asione kama wanamnyonya Sana, wamemtoa mbali na ni halali Yao kumfaidi mana na yeye anafaidika....konde mboy hawez kumfikia hata barnaba classic, lebel ndo inamnyanyua
 
Halina ubishi Harmonize ni msanii mkubwa tanazania kupita wote.
 
mavoko hakuwa hata na collabo hapo Kenya unamlinganisha na harmonize?
 
Atoke apotee.... mi show yake siwezi kwenda kama hana wasanii wengine hasahasa wa WCB.
unaongea utazani kutokuenda kwako kutampa faida hasi wala chanya wewe kwake ni kama Pampas aliyoitupa Malaya alipomaliza MP.
 
Barnaba ni msanii?
 
wewe jamaa kwangwaru jumlisha the uchafu wote wa barnaba
 
Sijui kwanini nimefananisha miandiko hii na kugundua kama mwandishi ni mtu mmoja
 
Harmonize hana uwezo wowote label inambeba kwanza sielewi kama anastyle yake mwenyew
 
wewe jamaa kwangwaru jumlisha the uchafu wote wa barnaba
Wewe unamjua Barnaba unamsikia, kasilikilize washa ya barnaba alafu ipe opportunity zote kama ilivyopewa kwangwaruu alaf urudi hapa, istoshe barnaba anaimba live na saut yake ni ileile kama unavoisikia kwenye audio ndo anavyoimba live, kitu ambacho harmonize hawez....harmonize aendelee kubaki WCB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…