Harmonize huku ni kulewa sifa sasa

Nimependa Jana Dullah kwenye planet bongo alivyogusia hili jipu na majibu ya uongozi wake...

Nadhani ni wakati harmonize anatakiwa kujitambua na kujirekebisha. Nimependa sana personality ya Raymond, harmo ajifunze kitu pale... Afu hata Diamond nae anakatatizo kidoogo kwenye kuongea, japo anabadilika taratibu anatakiwa awe mfano mzuri zaidi ya alivyo hivisasa maana kuna vitu visivyo na umuhimu sana kuviongelea kwenye media unakuta kaongea..
 
Diamond mwenyewe alihadithia jinsi gani alivyomtongoza Zari. Mambo mengine sio ya kuongea kwenye TV, unaonekana korongwee.
 
Huyu dogo harmonize ana undugu na wale madogo wa yamoto band? Maana wamefanana kichiz
 
Duuuh amaa mpo kumnyea leo huyo dogo, inatosha basi
 
Mmnnnh me kwel sielewi yule jamaa anachoimba. Na atachokwa karibuni tuuuuuuu
 
Ndo kwanza ametoka mwaka jana.... ana muda wa kujifunza mengi so tusimuattack as if we are dealin with a big fish...

Hana hata mwaka tokea ametoka, tumvumilieni dogo
 
Yule bwege hata sijui anaimbaga nini ila ndio hivyo tena watanzania tushakuwa kama manyumbu akionekana diamond tu kwenye wimbo basi huo wimbo watu watauaabudu mpaka basi!
haha..mkuu hata mimi style yake ya muziki siielewi iko kama mdumange wa wagosi wa kaya!
 
Ndo kwanza ametoka mwaka jana.... ana muda wa kujifunza mengi so tusimuattack as if we are dealin with a big fish...

Hana hata mwaka tokea ametoka, tumvumilieni dogo

Mkuu anatakiwa apelekwe hivi hivi maana ukihoji anavyokabwa koo inatakiwa uhoji pia kuwa ameanza tu mwaka jana inakuwaje anapata support kubwa hivi ndani na nje ya nchi?? dogo anapata support kutoka kwa mastaa wakubwa nje ya nchi, hadi kufikia kutrend Naija wimbo unasumbua.

Afu kuna kakitu kengine huwa wanazingua hadi na Diamond mwenyewe, kwenye kupost vitu kwenye social media typing errors kibao kwa kiswahili hadi lugha ya wenzetu, kwenye L unakuta R hahahaha ni vitu vidogo visivyohitaji kusomea kwa jinsi walivyo ni umakini tu ni kama huwa wanafanya vitu huku wakiwa wanafukuzwa..

Na diamond kama anapitia hapa inuhusu hii, anakamtindo ka kuandika post zake kwa kiingereza utafikiri wote tunakijua (tena kingereza chenyewe cha kubabaisha) ila ikitokea anaomba support kwenye wimbo mpya au kitu kikubwa anaweka kwa kiswahili.. Afu unakuta anaicopy post kupeleka Facebook au twitter na tag ya wrong account bila edit yeyote maana kama harmonize insta a facebook majina tofauti..

Hawa watu wanafanya vitu vikubwa hadi vilivyo nje ya uwezo wa kawaida, ila mambo madogo kama haya hawaimprove
 
Nitoe mimi mkuu,nimewahi kuuona huo wimbo mara moja kwa TV sikuelewa wameimba makorokocho gani hadi leo siujui hata neno moja.
Apia....
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…