Huijui music industry ya Tanzania wewe, kwahiyo kaa kimya! Na hapa hatuzungumzii nani anaingiza pesa na nani haingizi pesa! Narudia, huijui music industry ya Tanzania!!!
Eti kufeli kwa Mavoko! Huyo Harmonize amefikia level gani kulinganisha na level ambayo alifikia Juma Nature?! Je, baada ya Nature kutoka kwenye mikono ya wanaojua fitina za muziki wa Tanzania alifanya nini baadae?!
Huyo Harmonize amefikia level gani ukimlinganisha na Jide?! Je, unaweza kumlinganisha Jide aliyekuwa kwenye mikono ya wanaojua fitina za muziki wa Tanzana na Jide mwenyewe?!
Hivi kwa kipaji Harmonize unaweza kumlinganisha na Ruby?! Baada ya Ruby kutoka kwenye mikono inayojua fitina za music industry ya Tanzania alifanya nini?!
Hivi kama kweli unaujua muziki unaweza kumweka kapu moja na Aslay au Beka Flovor?! Nani kati yao ana-shine?!
Narudia, huijui tasnia ya muziki! Kwamba eti unaifahamu WBC in and out mimi hainihusu! Hata Asma Khan na mwenyewe anaijua WCB in and out! Sasa endeleeni kumjaza kama hajarudi kulima kulima ufuta Mtwara! JF hii hii naikumbuka ilivyokuwa inamjaza Ruby lakini kama kawaida, watu tukasema hapa acheni kumjaza Ruby! Kila mmoja sasa, pamoja na watu aina yako wanafahamu Ruby aliishia wapi!!!