Harmonize lisemwalo lipo, ila kabla ya kutoka WCB fanya ili

Harmonize lisemwalo lipo, ila kabla ya kutoka WCB fanya ili

Tunasikia habari mtaani kwamba Harmonize na menejimenti ya WCB Wasafi haziivi kwa sasa. Lisemwalo lipo na sisi tuliopembeni tukiunganisha matukio tunaona kabisa kuna kitu hakipo sawa japo wenyewe wanakanusha.
Anyways sio dhambi kabisa Konde kuwa na maisha mapya nje ya Wasafi maana ndio kukua huko.
Ila kabla hajatoka Wasafi tunaomba athibitishe kitu kimoja kwa mashabiki. Afanye hitsong bila ya kumshirikisha Diamond.
Sote tunajua na wataalam wa muziki wanajua Harmonize mpaka sasa ana hitsongs mbili tu kwenye maisha yake ya muziki na zote yupo na Diamond, nyimbo ya "Bado" na "Kwangwaru" zaidi ya hapo amewai kuwa na nyimbo nzuri ila hazikuwa hitsongs.

Harmonize prove us wrong..bila hivyo nje ya WCB utakuwa kama Mavoko tu.
ccm washamununua,
 
Umejuaje haziivi?, Mbona juzi mwenyew kawadiss waandishi kuhusu hizo shutuma

Kasema WCB kwake ni familia,hakuna harmoniz kama hakuna WCB,pia amesema Diamond kwake ni Baba yake..so mtoa mada acha kukuza negativity

Ndo yule mwandishi aliyepewa kubwa na harmo
 
Niliona ana furaha hata heshima wanampa kubwa maana yeye aliingia wa pili kutoka mwisho diamond ndio alimalizia kuingia walipishana kama dakika 10..nadhani ajipe kama mwaka mwingine akue zaidi ndani ya WCB ndio atoke akaanzishe kitu chake
kwanini unasema ivyo?
 
Kuwa na furaha hakumzuiyii mtu kuamua kwenda kuanza maisha mengine pengine.
 
Uzuri siku hizi WCB wanashindana wenyewe,sometimes si lazima wakukubali direct kuna wengine wanakukubali indirect.
 
Inawezekana asiwe na 'nyimbo za Taifa' nyingi, ila Harmonize ana nyimbo nyingi nzuri (Hana nyimbo mbaya), kwa sasa ni mkubwa kuliko Mavoko, so usitegemee kwamba akitoka atakuwa kama Mavoko, Harmonize namuweka level za Ali Kiba. Pamoja na hayo, simshauri kabisa kutoka WCB, hii bongo naijua kwa fitna atajuta[emoji3], pia backup ya Diamond inamuongezea kitu
 
Niliona ana furaha hata heshima wanampa kubwa maana yeye aliingia wa pili kutoka mwisho diamond ndio alimalizia kuingia walipishana kama dakika 10..nadhani ajipe kama mwaka mwingine akue zaidi ndani ya WCB ndio atoke akaanzishe kitu chake
sure kabisa anahitaji mda kidogo ili akomae.
 
Kwangwaru ilikua nyimbo kubwa kuliko nyimbo yoyote ya Ali kiba
Ulizaliwa kijijini hakuna radio?hakuna ngoma kubwa kwenye Bongo flavor kama Cinderella mpaka Sasa...Mondi mwenyewe aliimba
 
Ulizaliwa kijijini hakuna radio?hakuna ngoma kubwa kwenye Bongo flavor kama Cinderella mpaka Sasa...Mondi mwenyewe aliimba
umevuta nini ?
kuiimba diamond ndio ukubwa wa ngoma au ??
 
Aliyoandika Leo kumpongeza Boss Wake kama uliyaona tokaa Leo utaacha kuwa unaropoka
 
Back
Top Bottom