Harmonize naye ni mafia. Cheki alichomfanyia Angela

Harmonize naye ni mafia. Cheki alichomfanyia Angela

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Baada ya Konde kulia mbele ya media ku justify ubaya wa mondi, kumbe nae alimfanyia Angella [emoji23][emoji23]


"Sikuwahi kuwa na mimba ya Harmonize wala hatukuwahi kuwa kwenye mahusiano na hakuwahi kunitongoza hata siku moja. Ni kweli walichukua account za YouTube na nyingine lakini account yangu ya Instagram waliniachia hawakuwahi kuichukua wala hawakunichaji pesa yoyote, na hata nilipoondoka hawakunipa hata senti tano ya kuanzia maisha[emoji24]."

"Baadae walinirudishia account zangu zote, na kwasasa zinanisaidia sana, nawashukuru sana kwa hilo[emoji120] namshukuru Mungu sasa hivi pesa zote za nyimbo zangu zinaingia kwangu moja kwa moja, angalau naishi maisha ya amani, siyo kama zamani, siwezi kusema napata shilingi ngapi lakini Alhamdulillah napata kitu tofauti na zamani."
1687586348839.jpg
 
Sikuwa na chochote, watu wote waliokuwa wananichekea mwanzo walinikimbia sikuwaona, nilikuwa nashinda njaa, nakaa asubuhi mpaka usiku sijala chochote wakitokea wasamalia wema wananisaidia pengine saa tano usiku ndiyo nakula, yani nilikuwa nakosa kabisa hata miatano nilikuwa sina na hapo nilikuwa bado nipo ndani ya mkataba nilikuwa bado sijatoka"

"Siwezi kusema wamenionea au hawajanionea, ninachojua ni kwamba walifanya sahihi kulingana na mkataba ulivyokuwa unataka, kwasababu waliachana na mimi baada ya mimi kuchelewesha album yao ambapo mambo yaliingiliana, kipindi ambacho nilikuwa natakiwa niandae album ndiyo kipindi ambacho nilikuwa naumwa mguu nilikuwa siwezi hata kupiga hatua, nilijitetea lakini walishindwa kunielewa[emoji17]"

"
 
Na muda wote huo, sikuwahi kuonana na Harmonize, hakuwahi kuniita tuzungumze na hata nilipokuwa naenda BASATA hakuwahi kuja na mkataba ulipovunjwa nilimtumia meseji ya kumshukuru lakini bado hakuwahi kunijibu hadi leo. mwanzoni tulikuwa tunaishi vizuri lakini sijui kwanini alibadilika na hata sikuwahi kumkosea, ila mimi huwa naamini kila jambo lina wakati wake, kama Mungu alikupangia upite sehemu fulani ili ufike sehemu fulani, ndiyo maana sipendi kulaumu napenda kushukuru kwasababu Mungu hawezi kukupa changamoto ambayo huwezi kuishinda, alijua nitashinda ndiyo maana akanipa huu mtihani"- Anjella

Anjella ambaye jina lake halisi ni Angelina George Samson, ameongeza kuwa licha ya maumivu na mateso aliyoyapitia akiwa Konde Gang, hawezi kuacha kushukuru, anamshukuru Harmonize kwa kumtoa kwenye viwango vya chini na kumfanya ajulikane na aheshimike, ndiyo maana ameamua kuchora tattoo yenye jina la Harmonize ili kuonyesha umuhimu wake katika maisha yake, licha ya kwamba Harmonize hajamwambia chochote baada ya kuona amechorwa.
 
Sehemu ya pili (ll)

Baada ya konde kulia mbele ya media ku justify ubaya wa mondi....kumbe nae alimfanyia angella [emoji23][emoji23]


"Sikuwahi kuwa na mimba ya Harmonize wala hatukuwahi kuwa kwenye mahusiano na hakuwahi kunitongoza hata siku moja. Ni kweli walichukua account za YouTube na nyingine lakini account yangu ya Instagram waliniachia hawakuwahi kuichukua wala hawakunichaji pesa yoyote, na hata nilipoondoka hawakunipa hata senti tano ya kuanzia maisha[emoji24]"

"Baadae walinirudishia account zangu zote, na kwasasa zinanisaidia sana, nawashukuru sana kwa hilo[emoji120] namshukuru Mungu sasa hivi pesa zote za nyimbo zangu zinaingia kwangu moja kwa moja, angalau naishi maisha ya amani, siyo kama zamani, siwezi kusema napata shilingi ngapi lakini Alhamdulillah napata kitu tofauti na zamani"
View attachment 2667042
Story ile ile inajirudia. Mond na ruge, harmo na mond, angela na harmo.
Mnyonywa akipata chance naye hunyonya so mnyonyano...
 
Story ile ile inajirudia. Mond na ruge, harmo na mond, angela na harmo.
Mnyonywa akipata chance naye hunyonya so mnyonyano...
Katika kitu ambacho nashukuru wazazi wangu ni kunilea kwa kujitambua. Siwezi hata siku moja kupoteza muda wangu kufuatilia ujinga unaofanywa na watu kama hawa. Nitaanzaje kufuatilia ni kahaba yupi anatembea na kipanga yupi?
 
Katika kitu ambacho nashukuru wazazi wangu ni kunilea kwa kujitambua. Siwezi hata siku moja kupoteza muda wangu kufuatilia ujinga unaofanywa na watu kama hawa. Nitaanzaje kufuatilia ni kahaba yupi anatembea na kipanga yupi?
[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom