Harry Kane:Ni wakati wa Real madrid kuachana na Benzema na kumsajili Harry Kane

shevadon5

Senior Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
195
Reaction score
188
Kichwa cha habari kinajieleza ni wakati wa timu ya Real madrid kuvunja benki na kumsajili harry kane aje kusaidiana na Ronaldo katika kuondoa ukame wa magoli ambao timu unaikabili kwa sasa hivi kuliko kuendelea kua na mzigo kama benzema.
 
Ronaldo nae umri unamtuoa mkono mkuu...wasajili tu vizuri hawa jamaa
 
Akili za Zidane kumuuza Morata ili kumbeba Mfaransa mwenzie zinamtokea puani
 
Zidane abadili mbinu.

Yani akina penaldo ni kujificha kwenye box, wanasubiri cross zipigwe waruke kupiga vichwa!

Tofauti na hapo hawana la ziada!

Endeleeni kukariri, I see a trophyless season for you madridiots!
 
Kabisa mfaransa naye kashindwa kubebeka kabisa msimu huu.
Unalikumbuka goli la kwanza la super cup ya Spain pale camp Nou 2017?.Unakumbuka Benzema alichimfanya yule beki siju ni Pique sijui nani? Hata hivyo Benzema hajawahi maliza msimu bila goli 20.
 
Hicho ndio kinaenda kutokea. Daniel Leavy mmiliki qa club ya Spurs anajua sana kuuza wachezaji. Modric na Bale. Kuanzia january hii utaona media zitakavyo anza kumpa shavu Kane. Oooh Kane hauzi hata kwa £200m!

Maneno mengi mwisho Perez anaingiza kichwa anapigwa pesa.
 
Ronaldo ndio tatizo namba moja Real madrid. Kwaiyo wakuondoshwa mwanzo ni ronaldo wengine watafata.
 
Tottenham wamewauzia real Madrid ,modric na bale na wamewapa Madrid uefa champion Mara tatu,Tottenham ndio kwanza wamefanikiwa kufika 16 bora,sasa hapo nani kapigwa
 
Tottenham wamewauzia real Madrid ,modric na bale na wamewapa Madrid uefa champion Mara tatu,Tottenham ndio kwanza wamefanikiwa kufika 16 bora,sasa hapo nani kapigwa
Soka biashara wewe. Linapokuja swala la pesa hakuna club itaacha. Madrid wakifika bei wanapigwa pesa spurs wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo. Wapo wengi tu. Huko Amerca kusini ufaransa na nchi za balkani.

Atletico madrid walimuuza Falcao na pengo akaziba Costa. Wakamuuza Costa pengo akaziba Greizzman.
 
Michael Owen
David Beck hawa Waingereza waliweza kutoa walichokusudiwa pale madrid?

Madrid ni one man team Mfano game na Barcelona Cr7 alikua nje ya kiwango siku ile hata Kwasi au Shaibu Ninja wa Yanga wangempiga pini Sikuona haja ya kuendelea kuwepo ndani ya uwanja angetoka mapema tu Bale azame ndani na yeye pia ni Selfish mnoo.

Hary Kane kama atawezana na Philosophy za Zidane basi atakua mchezaji mzuri ila kucheza kwake vizur ni Vema Ronaldo apigwe mnada la sivyo ndo yale mambo ya mafahari wawili hawakai zizi moja.
 

Mzee vipi unatizama vizuri mpira lakini? One man team ??? Mchango wa ronaldo ni mdogo sana kwenye real madrid.
Akiwemo asiwemo atharti yake haionekani kabisa.
 
Wachezaji wa EPL hawatabiriki. madrid wasijiroge kumnunua kane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…