Harry Makange wa Channel 10 Afariki kwa ajali

Harry Makange wa Channel 10 Afariki kwa ajali

kapuchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Posts
268
Reaction score
163
wana JF nimepata taarifa muda si mrefu kuwa ndugu yetu Harry makange mtangazaji yule wa Channel ten amepata ajali mbaya ya pikipiki alikuwa anatoka nyumbani kwake asubuhi kule Kibaha akielekea kazini.

naomba mwenye taarifa kamili atupe habari za uhakika.
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi nimesoma kwa Michuzi na kupata taarifa kwamba mpendwa ndugu yetu HERRY MAKANGE hatunaye tena,amefariki baada ya kupata ajali ya pikipiki jana mchana akitokea Kibaha kuja Dar....RIP Mpiganaji mwenzetu Herry
 
Amegongwa na lori la mchanga akwia anaendesha pikipiki, amefarika dunia on the spot pamoja na mtu aliyekuwa amempakia. nadhani Channel ten watatoa taarifa zaidi.
Mungu amrehemu
 
Natoa pole kwa ndugu na marafiki wote wa marehemu.Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Harry,
RIP,HUJAMALIZA HATA MIEZI MIWILI YA NDOA YAKO,MUNGU KAKUITA.
MUNGU AMTIE NGUVU MKEO JANE NA WAZAZI WAKO KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
 
😀 harry makange wa channel ten apata ajali

Kapuchi:
Sijui unashangilia nini kwa Harry kupata ajali, ambayo imeondoa maisha yake...! Utu upo wapi? Mtu kapata ajali wewe unakenua meno!

RIP Harry Makange
 
Ni kijana mpole, myenyekevu na wajihi mwema. Ama kweli "wanaopendwa na wengi hufa wangali vijana"R.I.P Harry Makange.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina! Pole kwa wafiwa wote!
 
Kapuchi:
Sijui unashangilia nini kwa Harry kupata ajali, ambayo imeondoa maisha yake...! Utu upo wapi? Mtu kapata ajali wewe unakenua meno!

RIP Harry Makange

Hata mimi nimeshangaa jamaa anakenua mimeno kwenye swala hili. Natumaini atatueleza nini maana ya kukenua meno wakati taarifa anayotoa ni ya ajali. Inawezekana hakufahamu kama amebofya kwenye mikenuo ya meno.
 
Kapuchi:
Sijui unashangilia nini kwa Harry kupata ajali, ambayo imeondoa maisha yake...! Utu upo wapi? Mtu kapata ajali wewe unakenua meno!

RIP Harry Makange
Kibs najizuia kucheka sikuwa nimeona kapuchi anavyokenu....RIP Herry makange
 
ajali tatu ndani ya mwaka mmoja si kitu cha kawaida!!!! RIP Heri
 
Kawaida gani kupata ajali wakati kuna watu hawapati ajali kabisa. Inaonyesha kiasi gani hajui kuendesha pikipiki au uzembe bara baranai
 
Dah mwenzenu hata sielewi, huyo aliyekenua ni nani? Hivi aliyepata ajali kafa au yuko mahututi anasikilizia habari yake???
 
Hivi nyie mnaolalamikia hiyo icon ya kukenua, huwa hamjui kuwa mtu anaweza kuwa amechanganyikiwa na mshtuko wa taarifa yenyewe akabofya kusikotakikana,mbona hamna dogo nyie!! si mngemwambia moderator aweke sawa.

mie niko majonzini! hata hivyo hakuna icon inayoonyesha mtu anadondosha machozi ningeiiklick,msinitaabishe!!

RIP- Herry
 
Back
Top Bottom