Leo jioni nimetembelewa na rafiki yangu ndugu Haruna Mbeyu. Nimemjua Haruna bado mtoto mdogo wa shule
Miaka mingi hayupo lakini hapungui Tanzania. Haruna ana ila moja. Kila akipata mtu anakuja Dar es Salaam kutoka London atampa vitabu aniletee. Leo kaja nikaona ndiyo nafasi yangu.
Nikakumba baadhi ya vitabu alivyoniletea nikamuomba tupige picha nimevibeba.
Kanikubalia. Usishangae.
Haruna toka udogo wake ni Educationist. Akiwa kijana mdogo sana alifungua shule mtaani kwake. Shule hii ipo hadi hivi sasa watoto wanasoma.
Almaarufu meya wa muda mrefu. Cheo cha heshima wenzie wa diaspora wamepatia kwa kujitoa kwa jamii bila kuchoka.
Mh. Naibu Spika, Job Ndugai (wa kwanza kushoto), akipokea nishani kwa niaba ya Mama Salma Kikwete kutoka kwa Dk. Mohammed Zaharani. Wakiangalia kwa furaha ni Mh. Beatrice Shelukindo, Bi Mariam Mungula na Ndg. Haruna Mbeyu