Sasa nikubali kuffuata wanavyotaka wao au niwaachie mtoto wao?
Swala la harusi liantegemea na mfuko wako,
Mnapofunga ndoa kukiwa na sherehe nayo ina raha yake, mnaweka kumbu kumbu nzuri kwa watoto wetu mtakaokuja kupata baada ya hiyo ndoa yenu, Kama mfuko unakuruhusu fanya sherehe bana, hiyo ndio raha ya harusi.
Kama kweli umempenda huyo msichana jitahidi tu ufanye sherehe. Sherehe isiwe sababu ya kumuacha binti wa watu.
Bravo BroooooooooMwiba kwa nini hutaki sherehe ya harusi? Jibu la swali hili litatusaidia kukupa ushauri muafaka zaidi.
Kwa maoni yangu sherehe inafanywa kwa sababu kadhaa. Kwanza ni kama alama ya kuonesha 'umuhimu' wa tukio lililotokea (iwe ni wanandoa,wazazi, ndugu am hata marafiki). Pili, ni kuonesha 'furaha' kwa tukio la kufunga ndoa.Tatu unaweza kusema ni kama 'ushuhuda' (kumbuka si watu wengi wanahudhuria ndoa kanisani,bomani nk) kwamba wawili hawa sasa ni mwili mmoja. Sababu nyingine ni wanandugu 'kukutana' na 'kufahamiana' (ingawa sio effective kihivyo!). Na mwisho sherehe inatoa nafasi kwa watu 'kuwapongeza maharusi pamoja na wazazi wao' (si rahisi watu wenu wa karibu kila mmoja kuja nyumbani kwenu kuwapongeza!).
Mara chache sana kusikia mtu hataki sherehe isipokuwa kwa sababu maalumu sana (ukata, siku ya harusi imeingiliana na msiba wa ndugu wa karibu, wanandoa wamesha kaa kinyumba kwa muda mrefu nk).
Nakutakia fungate njema.
Kweli ,ni furaha,ushuda,kumbukumbu na menginetele ,ila yote ni gharama ,siku hizi kwanza imekuwa kama mtaji ,mahari hayapungui chini ya milioni mbili ,sijui wanafikiria watu wote wanafanya kazi buzwagi ? Na halafu mbali ya yote ,nawatarajia watanichuna mimi tu,dalili nimeanza kuziona ,tatizo wakianza na madai na halafu huna kitu mfukoni watakuona bahili ,jambo ambalo nalichukia kuliko yote duniani ni kuonekana bahili ,na siku hizi walaji wamegundua haya mambo ya kuunda kamati ,yaani wameingiza mambo ya ulaji wakiserikali katika mambo ya harusi , wanazidi kutumaliza.
Kutokana na ushauri wenu huo wa kutosana nitauangalia lakini naona chance ni ndogo sana kama 25% hivi. Au nitawambia chakula tutachemsha mihogo ka sufuria tatu na kauzu ,tunalinda utamaduni wa Mtanzania ,mambo ya kiarabu sijui pilau haluwa ,hamna pilau wala haluwa. Kwanza mambo ya kamati sikubaliani nayo ni wizi tu.
Kamati kwenye harusi imehusu nini ,kama sikuchomoana ?
..........kuunda kamati ,yaani wameingiza mambo ya ulaji wakiserikali katika mambo ya harusi , wanazidi kutumaliza.
...................Kwanza mambo ya kamati sikubaliani nayo ni wizi tu.
Kamati kwenye harusi imehusu nini ,kama sikuchomoana ?
harusi haina maana iwe ni sherehe kubwa za kifahari zisizo za lazima angalieni kipato chenu ,sherehe kiasi inatosha lakini kimya kimya babu Akaaa,mie siungi mkono hilo,kwani unaiba,tutangazie tujue kwamba sasa umejiandikisha rasmi katika majamboz au vipi!Halo hii mada imekuja mahali pake kabisaaaaa! Maana saa chache zilizopita tulikuwa na kikao cha harusi ya mdogo wangu inayotarajia kufanyika mwezi Novemba 2009.
Kwa kweli naweza kuungana na mtoa mada kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa sherehe ya harusi. Kwangu binafsi naweza kusema sherehe isiwepo kutokana na mifano hai iliyonikuta hivi punde.
Tumejitahidi kutoa mahari ambayo jumla yake imegharimu sh. 1,014,000 sasa imefikia wakati iundwe kamati ya sherehe hiyo wanasema inatakiwa niwe angalau sh. 600,000 na nyingine kuwalisha na kuwanywesha wanakamati hao kwa gharama nyingine tofauti na hiyo laki sita, kwa haraka haraka inatakiwa niandae jumla sh. 1,200,000.
Je, kwa hali kama hii sherehe itafanyika? Maana uwezo wetu ni mdogo sana.
Kwa mfano kipato changu ni sh. 120,000 kwa mwezi. Ndio maana mtoa mada akauliza hilo swali.
Wengine waendelee kuchangia hoja.
Jamani sijui nianze kwanza kulia halafu nichangie hoja hii.mkuu kamati muhimu sana, coz kamati ndio inafanya maandalizi yote ya shughuli, ingawa kweli wajanja pia wanakuwamo kwenye kamati hasa pale mnapopiga mahesabu ya juu halafu mwanakamati anafanya usanii, mfano mnapiga mahesabu kadi moja sh. 1000, kwa kadi 200 itakua 200000, sasa atatokea mwanakamati msanii atasema mumpe kazi hiyo, ataenda kutengeneza kwa 700, hapo atachukua cha juu sh. 60000! kiulainiii.
ukija kwenye faida za kamati, utakuta kwamba huwezi kufanya kila kitu mwenyewe kwa ajili ya shughuli ya harusi au whatever, hivyo unahitaji watu wakusaidie, watu wenye ujuzi na uzoefu, unaweza usifahamu kitu gani kinapatikana wapi na kwa gharama nafuu, then kwenye kamati lazima kutakua na mmoja anafahamu, mwisho wa siku shughuli itakwenda sawa.
chukulia mfano hauna kamati, mkajigawa tu dada, kaka, wajomba, shangazi unadhani hapo shughuli itakwenda?, maana wengine tutatoa laki 2 zetu za mchango tutaambulia bia moja au tusilambe kitu!, eeeh si mtakua mnagawana kindugu!.
Jamani sijui nianze kwanza kulia halafu nichangie hoja hii.
Yaani juzi juzi nimeitisha wanandugu na baadhi ya watu ili tuunde kamati ya harusi
Nimewaambia nina shilingi 300,000 tuuuu mnisaidie ili tufanikishe harusi hii. Sasa badala yake wananiambia haitoshi kabisa kuitisha kamati. Halafu wakati huo huo wanasema inatakiwa niilishe kamati na kuinnyesha mpaka walewe na gharama ya kulisha watu zaidi ya 50 na kuwalewesha bia si mchezo.
Ndio maana nasema hakuna umuhimu wa sherehe. Labda tuandae sherehe ya kunywa chai na maandazi.
aisee, pole sana!
kwanza kama unaishi dar mkuu kilo 3 haitoshi kwakweli, hata ukumbi hupati kwa kilo 3 ndani ya dar, atleast ungekua na kilo 5.
pili wanandugu usiwajaze, wengi miyeyusho tu, hawako serious hata kidogo na watakulostisha, tafuta marafiki zako wale wa karibu na ndugu wachache wenye akili, isitoshe kwenye kamati inatakiwa mwanakamati atoe hela ya uchakavu, sasa hapo kwenye uchakavu kuna wengine wanakunywa bia 5 halafu wanatoa 2000 upumbafu mtupu!, kunywa kadri ya pesa yoko bana.
Ina maana nagharamia peke yangu? Si hao wengine wanichangie ili zitimie kukodi ukumbi na mambo mengineyo? Karibuni Mbeya jamani.hata ukumbi hupati kwa kilo 3 ndani ya dar