Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Wateja wa chumba hiki cha mahaba napenda kuwauliza ili kujua kama kuna umuhimu wowote ule wa kufanya sherehe za harusi ,au ni kuuoa na kuondoka bila ya sherehe zozote zile ? Na kuna siri yeyote ile ambayo inapelekea kufanywa sherehe za harusi ? Kuna seemu nimetaka kuoa ,mimi nimewambia sihitaji sherehe za aina yeyote ile .ila upande wa mtoto wa kike wao wameshikilia ni lazima ifanywe sherehe ,nimetishia kuachana nae ,ila narudi hapa kutafuta ushauri unajua JF ina wenyewe ,na bila ya shaka majadiliano ya hapa huwa mara zote yananinufaisha. Sasa nikubali kuffuata wanavyotaka wao au niwaachie mtoto wao ?