Harusi na Michango yake chimbuko jipya la mitaji ya biashara Kwa vijana

Harusi na Michango yake chimbuko jipya la mitaji ya biashara Kwa vijana

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Nimeona niongelee hili jambo, kwani linatrend sana, tatizo la ajira limekuwa kubwa sana, kiasi kwamba vijana wengi wameshindwa kuajiriwa au kujiajiri Kwa ukosefu wa mitaji.

Nafurahi pia Kusema kuwa ,utaratibu uliopo Tanzania wa kuchangiana Kila Kijana anapotaka kuoa imekuwa ni mkombilozi Kwa vijana wengi, kwani vijana wengi wameoa na wanafanya biashara zao Kwa kutumia michango waliokusanya kupitia ndoa walizotangaza na kufungua Grupu wasap.

Michango ya Harusi imekuwa ni Faraja Kwa vijana kwani imeweza kuwainua kiuchumi na kupunguza mzigo wa Serikali kutoa ajira.

Ninatoa Rai Kwa wananchi wa Tanzania kuenzi na kudumisha utaratibu huu kwani japo unaumiza wachangaji unasaidia pia kudumisha uchumi
 
elimu inayoandaa vijana na white collar jobs inabidi iwe pyramid. each stage as you go up gets tougher and tougher to get out of.. ndio maana nchi nyingine wana trade schools and shule za skills mfano wa VETA. Cha ajabu hapa kwetu mamba ni bwerere,ukianza darasa la kwanza probability ya kumaliza chuo sasa hivi ni asilimia 95.
 
Harusi za wengine zisiwe kero kwa wengine.

Imagine kima cha chini utachangia laki moja, kwa mwaka una kadi lukuki yani utapotezea nyingine lakini utakuta shilling million moja inaende kwenye michango ya harusi.

Hapo bado school fees, vyama vya kijamii, kulisha familia, na ndugu wanaojitafuta au wazee wanahitaji uwape financial support kwakweli hii siyo sawa, kuna sehemu tumepotoka.

Zamani nakumbuka mnakaa miaka husikii harusi yani akikupa kadi au kwenda kwenye kikao unatowa mchango wa nguvu wa kujimaliza maana yalikuwa ni matukio ya nadra sana kwenye jamii, lakini kwa sasa is too much wenye kumbi wanajipigia pesa tu wanakwambia ukichukuwa ukumbi chakula na mapambo ulipie kwao ni wizi mtu na kuwanyima watu choice.
 
Kuna harusi eti wanakamati wote mchango ni 350,000 kila mtu
Kibaya zaidi hata sikuwaomba waniweke kwenye kamati,nimeomba kujitoa wanatumia nguvu nyingi nibaki
Hapa kuna mawili, huenda hii kamati wote mmechaguwana uchumi wenu upo vizuri na mnajuwana hata wakisema milioni ni sawa tu.

Lakini mimi bajeti yangu ya kuchangia harusi ni shilling laki moja tu unless kwa mazingira maalum na upepo ukiwa umevuma vizuri na ni familia ninaiheshimu hata laki tano natowa lakini zingatia cha kwanza upepo mimi sina mshahara sijaajiliwa popote pale.
 
Hapa kuna mawili, huenda hii kamati wote mmechaguwana uchumi wenu upo vizuri na mnajuwana hata wakisema milioni ni sawa tu.

Lakini mimi bajeti yangu ya kuchangia harusi ni shilling laki moja tu unless kwa mazingira maalum na upepo ukiwa umevuma vizuri na ni familia ninaiheshimu hata laki tano natowa lakini zingatia cha kwanza upepo mimi sina mshahara sijaajiliwa popote pale.
Unawaambia mapema kabisa wazingatie Neno -'Upepo'
 
Pesa ya Michango huwa inaishia kwenye kufanya sherehe na kama ikibaki huwa ni kidogo tu haiwezi kukutoa kimaisha
 
Mkuu Yani unakomaliwa kama deni Wakati kadi yenyewe uliikuta tu imeletwa nyumbani ukiangalia ni ndg wa karibu hapo anajua unafanya kazi Gani na unaingia trh ngapi mshahara wengine wale tunafanya nao kazi asee Yani kukwepa unashindwa kujikausha unashindwa. Mfano mwezi huu tulikuwa na bonus aisee utafikiri yeye ndo kahusika kuweka hii bonus halafu mbaya zaidi wanakuwepo wapambe/Chawa
 
Nina jamaa yangu baada ya harusi aliuza hadi gari, yupo kkoo. Yaani alichotegemea na alichopata sicho. Mzee kafunga milango kabisa.

Jamaangu Kuna wengine huwezi kwepa. Mfano shemeji Yako yaani kaka ake na mke wako unadhani usipotoa humo ndani Kuna Rangi utaacha kuitoa na wanawake wanavyopenda harusi vile halafu iwe ya kaka yake?
Hapo pagumu
 
Back
Top Bottom