Mna kazi kweli kweli, mimi nashukuru nimejiwekea utaratibu wa kutokuchangia arusi ya mtu yeyote labda ndugu yangu au mfanyakazi mwenzangu, tena kwa kiasi kidogo sana. kuna makaka wawili walioa kazini kwetu walinifurahisha sana tena, mmoja alirudi kutoka likizo tukamuona anaoendeza pendeza tukamuuliza mbona unapendeza kama umeoa? akasema ni kweli nimeona, haki ya Mungu hakuna alojua hilo sasa mtu tu kwa furaha unaamua kumnunulia zawadfi au kumsaidia chochote ambacho si lazima, mwengine yeye alioa akawaita watu 50 tu tena si lazima kuchangia, kwetu sisi pwani enzi hizo siku hizi nao wananza kuiga mambo yasi yao! mwali anawekwa nje ya nyumba na kesho yake mnajipiga na pilau au biriyani na maji ya kunywa arusi imehsa, you will hardly spend 1-5m to 2m tena huko ni kwenye higher side ..poleni sana, inabidi watu tubadilike.
Utakuta mtu anaumwa ugonjwa unaohitaji kuchangiwa mgonjwa apate matibabu au dawa, waLLAhi humuoni hata mtu mmoja, na akishakufa watu wanatoa ubani unajiula wanini? sasa ngoja ije arusi watu watachangia malaki na mailioni, au utakuta mtoto hana ada ya shule na ana akili sana ukiomba msaada watu kimya...TUNAKWENDA WAPI WATANZANIA? ujinga ujinga ujinga, ni vema kama mdau wa juu alipsema inabidi tuzibadili akili zetu la sivyo ni balaa.
Sometimes unakuta mtu unaombwa mchango na mtu anaeoa au kuolewa humjui eti? ! au sometimes mtu mnafahamiana kwa mbaali lakini utaona anakenua kumbe anataka kukuomba mchango! halafu KAMA DENI UTAPIGIWA SIMU NA KUKUMBUSHWA KILA SIKU, SICHANGII SICHANGII SICHANGIII