Harusi ya Vicky Kamata ni mil 96

Harusi ya Vicky Kamata ni mil 96

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
560
HAYAWI… hayawi sasa yamekuwa! Habari ya mjini ni maandalizi kabambe ya harusi ya staa wa Bongo Fleva na Mbunge wa Viti Maalum ( CCM) anayewakilisha Vijana Mkoa wa Geita , Vicky Pascal Kamata ikidaiwa kuwa shughuli hiyo itatafuna kiasi cha Sh . milioni 96,IJUMAA LAMNASA BWANA HARUSI Habari kutoka kwa chanzo cha ndani zilisema kuwa Vicky anatarajia kufunga pingu za maisha Mei 24 , mwaka huu na mchumba wake wa muda mrefu ambaye Ijumaa limemnasa aliyejulikana kwa jina la Charles Pai.

Ilidaiwa kwamba mwanaume huyo ni kigogo ndani ya kampuni moja ya huduma za simu hapa nchini. HARUSI YA REKODI Kwa mujibu wa mtonyaji wetu huyo ambaye naye ni miongoni mwa wanakamati , harusi hiyo inatarajiwa kuweka rekodi ya aina yake Bongo .

"Sijawahi kuona harusi ya kifahari kama ya Vicky , itafanyika tarehe 24 mwezi huu, ina siku chache tu, huwezi kuamini mambo yote yamekamilika," alisema mpashaji wetu . HOTELI YA NYOTA TANO Imesemekana kwamba baada ya ndoa hiyo kufungwa kanisani , shughuli itahamia katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro iliyopo Posta , Dar ambapo waalikwa watagonga mnuso wa maana na vinywaji vya kumwaga. Habari zilieleza kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa na mawaziri , wabunge wenzake , vigogo mbalimbali serikalini na baadhi ya wasanii wenzake.

Ilidaiwa kuwa bajeti ya shughuli hiyo imefikia kiasi hicho kwani Vicky anataka iwe ya aina yake. BAJETI MIL. 96 Kwa mujibu wa mwanakamati huyo, kwa bajeti hiyo ya Sh . milioni 96, Vicky atakuwa amevunja rekodi ya ndoa za mastaa zilizowahi kufungwa Bongo. "Nakwambia harusi ya Vicky haina mfano, itafunika harusi za vigogo na mastaa wengi, itakuwa ya aina yake.

Bajeti yake siyo ya kitoto . "Watu wengi wamemchangia, achilia mbali na kuweka hela yake yeye binafsi na mchumba wake, kitu kama Sh. milioni 40 . KUVUNJA UKIMYA NA UVUMI "Hakika mheshimiwa amejipanga kuvunja ukimya na uvumi mwingi juu ya maisha yake ya kisiasa na jamii inayomzunguka," alisema mtoa habari wetu na kuongeza : VIKAO NI DAR , DODOMA "Huwezi kuamini , vikao vingi vya harusi sisi wanakamati tunafanyia Dar .

Lakini mara nyingine tunafanyia Dodoma kwa sababu waheshimiwa wengi wanakamati wako huko. "Hata kwenye vikao watu wanakunywa na kula je, siku yenyewe itakuwaje? Unaambiwa msafara wa magari ya kifahari tupu na utakuwa kama wa rais ukiongozwa na farasi. VICKY ANASEMAJE ?

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimsaka Vicky kwa udi na uvumba ili kujua mchakato mzima wa harusi umekaaje lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa huenda ni kwa sababu ya kubanwa na vikao vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma huku bwana harusi akishindwa kutoa ushirikiano .

Hata hivyo, bado tunaendelea kumsaka Vicky au kama atasoma habari hii tunaamini anaweza kupiga simu kwenye chumba cha habari na kufafanua jambo lolote juu ya tukio hilo la kihistoria kwa maisha yake


attachment.php
 

Attachments

  • vik.jpg
    vik.jpg
    33.9 KB · Views: 7,379
Nilithani kuna kitu cha ajabu sana lakini hata sijaona, kwani mamilioni ya pesa yanamaanisha nini kwenye ndoa, watu tumeoa kwa mahari ya laki moja na nusu na sherehe ya harusi iligharimu shilingi laaki sita, nipo na mke wangu na tuna watoto wanne tunaishi kwa furaha sana kila siku
 
Ndio Tanzania ya Leo hakuna atakaehoji uhalali wa wapi yametoka hayo mamilion.
Nyuma yake kuna
1.Yatima wanateseka
2.Huduma duni za afya
3.Nyumba za walimu
4.Madawati hakuna
Any way kupanga ni kuchagua,muheshimiwa ameamua kutuonyesha ufahari wake walala hoi wa nchi hii.
 
Tumeshazoea,harusi gharama lukuki,furaha ndani ya ndoa=0!!!:hug:
 
Mimi mwanandugu, VK ni kama mwanangu( shangazi yake VK). Ni mambo ya kawaida sana kwetu, hata watotoyatima, wajane, madawati huwa tunatoa- ila tu wandishi wa habari hawapendikuandika mazuri.
Kweli kupanga nikuchagua na wengine huchagua kufungia ndoa Manzese hotel, huo ndo uwezo wao, mwingine huishia kanisani hata soda ''ntoho'' na Mungu anawabariki pia, ndoainadumu.
Another serious note; hii siyo ya kifahari- bali ni kasherehe kadogo ya kuwapongeza vijana wetu kwa maamuzi mazuri waliofanya, ni kabudget ni around USD 75,000

 
Ndio Tanzania ya Leo hakuna atakaehoji uhalali wa wapi yametoka hayo mamilion.
Nyuma yake kuna
1.Yatima wanateseka
2.Huduma duni za afya
3.Nyumba za walimu
4.Madawati hakuna
Any way kupanga ni kuchagua,muheshimiwa ameamua kutuonyesha ufahari wake walala hoi wa nchi hii.

Hujakosea mkuu. Waafrica tuna mambo sana aise. Acha tu!!!


The king.
 
Namwonea tu huruma huyo jamaa, Vicky si alikuwa mchepuko wa bw. Visasi! Asije kusema hatukumwambia, mwenzake anaozea Segerea hivihivi.
 
Kwani ameachana na bwana wake tunayemfahamu?

Maana nimeufungua huu uzi nikitegemea kwamba ni jamaa ameamua kurasmisha!
 
Mbona kawaida sana kwa status yake!!!!!!!?????
Mshahara wake kwa mwezi shilingi ngapi!!!????
Bunge la katiba kapiga ngapi!!!???
Hili la bajeti anapiga ngapi!!!????


Uswazi huku tunakamua mpaka za 40M na wachangiaji ni watu wa kawaida tu hawana social credo kama wanaomzunguka huyo bi harusi....
 
Nilithani kuna kitu cha ajabu sana lakini hata sijaona, kwani mamilioni ya pesa yanamaanisha nini kwenye ndoa, watu tumeoa kwa mahari ya laki moja na nusu na sherehe ya harusi iligharimu shilingi laaki sita, nipo na mke wangu na tuna watoto wanne tunaishi kwa furaha sana kila siku

Word ata hujakosea pesa makaratasi na siku hazigandi.
 
Mimi mwanandugu, VKni kama mwanangu( shangazi yake VK). Ni mambo ya kawaida sana kwetu, hata watotoyatima, wajane, madawati huwa tunatoa- ila tu wandishi wa habari hawapendikuandika mazuri.
Kweli kupanganikuchagua na wengine huchagua kufungia ndoaManzese hotel, huo ndo uwezo wao, mwingine huishia kanisani hata soda ‘’ntoho’’ na Mungu anawabariki pia, ndoainadumu.
Another serious note; hii siyo ya kifahari- bali nikasherehe kadogo ya kuwapongezavijana wetu kwa maamuzimazuri waliofanya, ni kabudgetni around USD7

Hata kuandika kwenyewe taabu kwelikweli!
 
Kwani ameachana na bwana wake tunayemfahamu?

Maana nimeufungua huu uzi nikitegemea kwamba ni jamaa ameamua kurasmisha!

itakuwa jamaa aliiruhusu hii kitu kwa mashart!
kwamba akiwa na hamu anytime anapiga mzigo laa si hvyo!.....
 
Back
Top Bottom