Harusi za wenye hela Samatta, Majizo, Lulu, Millard Ayo zipo simple hakuna sherehe. Ila Harusi za vijana hohehahe tunakabana michango

Harusi za wenye hela Samatta, Majizo, Lulu, Millard Ayo zipo simple hakuna sherehe. Ila Harusi za vijana hohehahe tunakabana michango

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
Habari wadau.

Najiuliza kwa nini vijana matajiri wenye hela wanafanya harusi simple zisizo na michango wala sherehe kubwa zisizozidi bajeti hata milioni mbili.

Mbwana Samatta alifunga ndoa akiwa anacheza mpira ulaya hakuna sherehe wala nini

Majizo mmiliki wa EFM alifunga ndoa na Lulu muigizaji mkubwa hakuna sherehe wala nini

Millard Ayo alifunga ndoa hakuna sherehe wala nini.

Mwana Fa akiwa amejipata alifunga ndoa simple bila sherehe kubwa

Ila vijana maskini wanapenda harusi kubwa na kusumbua watu michango.

Yaani nimeungwa grupu la harusi nimekereka kweli kweli
 
Habari wadau.

Najiuliza kwa nini vijana matajiri wenye hela wanafanya harusi simple zisizo na michango wala sherehe kubwa zisizozidi bajeti hata milioni mbili.

Mbwana Samatta alifunga ndoa akiwa anacheza mpira ulaya hakuna sherehe wala nini

Majizo mmiliki wa EFM alifunga ndoa na Lulu muigizaji mkubwa hakuna sherehe wala nini

Millard Ayo alifunga ndoa hakuna sherehe wala nini

Ila vijana maskini wanapenda harusi kubwa na kusumbua watu michango.

Yaani nimeungwa grupu la harusi nimekereka kweli kweli
Nadhani ungejishughulisha kwanza kujua bajeti za sherehe za harusi zao kabla hujasema hiyo kauli ya kwamba zilikuwa 'simple' tu.

Maana nahisi neno 'zilikuwa simple tu' umelipata kwa vile wao waliamua kukuonesha sehemu ndogo tu ya sherehe za harusi zao.

Ova
 
Ukiangalia ndoa nyingi zilizorushwa kwenye AZAM TV live zimekufa chalii kwasababu vijana wa siku hizi wameacha tamaduni zetu na kuvamia za wazungu ndoa ya ali kiba na za manara zote chalii licha ya kuwa live kama derby ya kariaokoo.
 
Back
Top Bottom