Hasara ipi ningepata nisingekuwa Mtanzania?

Hasara ipi ningepata nisingekuwa Mtanzania?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Nimekuwa najiuliza ni hasara ipi ningeweza kupata nisingekuwa Mtanzania au ni faida gani special ambazo napata kuwa Mtanzania. Nikitazama maisha ya nchi nilizowahi kupita naona zina fursa zaidi ya Tanzania kwa utafutaji mfano Malawi, Zambia, Botswana, South Africa, huku biashara zinalipa kuliko hapa kwetu ( kasoro Kenya hali huko ngumu)

2. Tukija siasa za nchi hizi ni safi kuliko za kwetu Tanzania ( huwezi kusikia kiongozi anawambia wananchi mimi ni mama halafu kundi kubwa la wajinga linashangilia( hakuna raisi mama wala baba, fanya kazi as rais) , kuleni kwa urefu kamba zenu, January to December nchi ni uteuzi tu na wanaoteuliwa ni walewale , mara kusikia kuna maridhiano ya vyama vya sasa, mara wapinzani kusifu utawala uliikuwepo (malema yule myiha awasifu ANC ) nikikumbuka jpm anasema ntawafyekelea mbali dah,

3. Mambo ya kijamii ukitoa ( Wamalawi ni washamba) Watanzania pia ni washamba sana, sisi ndio tunamini kila mtu aliyefanikiwa ni mchawi, fisadi nk,sisi ndio tunafanywa chochote na viongozi wa dini. Kiufupi huwa najiuliza sana ipi faida hasa ya kuwa Mtanzania ambayo mimi napata ( mimi ni mwalimu je nisengeweza kuwa mwalimu South Africa, ni mfanyabiashara vipi nisengefanya biashara huko Botswana ambako riba za mikopo zinafika asilimia hadi nne muda fulani, kilimo ninachofanya vip South Africa, Zambia nisingefanya , nisaidie wewe kipi unapata unahisi raia wa nchi nyingine hapati.
 
Kuna uraia wa ku asili, badilisha madesa tu mwalimu.. acha sie tukomae na Tz yetu!

Nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani - J Nature.
 
Kwani kwenye hizo nchi wamekukatalia kwenda kuwa raia wa huko? Kama hawajakukatalia mimi nakushauri uhamie huko fasta. Sisi tusiopenda ujinga tutakomaa na Tanzania yetu.
 
Wewe tatizo lako ni maridhiano tu, hayo mengine ni nyongeza tu. Unaweza kuhamia kwenye hizo nchi ambazo unafikiri ni bora kuliko Tanzania.
 
Watu kama wewe ni hasara tu kwa nchi yetu, ukihamia huko kwingine utakuwa umeipunguzia mzigo.
 
Unang'ang'nia nini Bongo Rudi J'burg zile hostel zilizojengwa na Makaburu bado hazijajaa wala usiogope Wazulu na chuki zao kwa wageni🙄
 
Back
Top Bottom