Hasara kubwa mbegu za alizeti (ASA)

Hasara kubwa mbegu za alizeti (ASA)

Oranoo

Member
Joined
Apr 11, 2020
Posts
56
Reaction score
184
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za Serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
 
Duh, labda kama hamkufuata maelekezo, ila hii ni ya kuwafikishia Wahusika wa Wizara.
 
Habari wana jamvi, naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Naona una hasira nao mkuu. Poleni sana ndo watafiti wetu hao
 
Hii ni hatari, hata wakifikishiwa taarifa watafanyaje na sisi wakulima tushapata hasara kubwa
Kama Mpo wengi nadhani mkiungana mnaweza kufidiwa...ali mradi tatizo liwe kweli limeanzia kwao.
 
Hapo hamna cha kufidiwa ni kujipanga tu upya, kazi iendelee
 
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Hizo sio hybreed mkuu. Ziko graded and packed tu. Mbegu hybreed inauzwa 130k kwa 2kg
 
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Bongo nyoso...full kutukana hasara...usikute Kuna kigogo mmoja alikuwa winga katika ununuzi na uuzaji wa mbegu
 
Alizeti halitaki mvua nyingi,Songea Kuna mvua nyingi,mvua nyingi inasababisha mafuta yawe kidogo.Inawezekana tatizo siyo mbegu ila ni wewe mkulima.
Ni kweli inawezekana sio mbegu kama jamaa kashavuna alizeti mwezi huu wa 5, ina maana alipanda kipindi cha mvua nyingi.
 
Songea siyo sehemu rafiki kwa kilimo Cha alizeti

Wengi mnalazimisha tu, huko kuna mvua nyingi Sana kitu ambacho zao Hilo halitaki.

Subiri watu wa Manyara, Dodoma na Singida waje watoe mrejesho ndio utaona utofauti mkubwa sana.
 
Mbegu ni mbaya sijawahi kuona, nilipanda Songea na Iringa ni kituko
 
Back
Top Bottom