SoC02 Hasara ya kujiajiri ilinifanya nisiamini vyombo vya dola tena

SoC02 Hasara ya kujiajiri ilinifanya nisiamini vyombo vya dola tena

Stories of Change - 2022 Competition

MAKALANDEI

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
4
Reaction score
2
Kujiajiri si jambo rahisi kama wengi wanavyodhani.Wanasiasa na viongozi wanasisitiza kujiajiri wakisahau wajibu wao wa kuweka mazingira wezeshi ya kujiajiri.Japo wakati mwingine tunawajibika kujiajiri kwa sababu ya ukosefu wa ajira uliopo.Andiko hili linalenga kuainisha uzoefu wangu binafsi wa ugumu wa kujiajiri katika mazingira halisi.

Nililipa kodi kabla ya kuanza biashara; Biashara niliyolenga kufanya ni uwakala wa miamala ya simu,na ili uweze kusajiliwa ni lazima uwe na 'Namba ya mlipakodi' na 'Uthibitisho wa malipo ya kodi' kutoka mamlaka ya mapato.Kilichonishangaza ni mamlaka kufanya makadirio na kutaka nilipekodi tena kodi ya mwaka mzima ili nipate 'Namba ya mlipakodi' na 'Uthibitisho wa malipo ya kodi' nilikwazika sana.Ilinilazimu kulipa kodi ya mwaka mzima kabla ya kuanza biashara ambayo nilitegemea kuanza mwezi wa kumi.

Hasara iliyonifanya nisiamini vyombo vya dola tena.Mara tu baada ya kuanza biashara nilitapeliwa kama shilingi 300,000 bahati nzuri nilimkamata aliefanya huo utapeli,nikaona ahueni.Nilipompeleka polisi sikuamini kilichonikuta.Mwanzo walionesha ushirikiano wakisema hawa tunawajua,pesa yako utapata wakaniambia njoo kesho.Kesho yake ilipofika nilienda sikumkuta mtuhumiwa na walinambia kawekewa dhamana huku wakinishauri kuachana na kesi hiyo kwani ina mlolongo mrefu na gharama nyingi.Nikafatilia sana lakini afisa upelelezi hakuonesha ushirikiano na kunikwepa kila mara.Ilifika wakati nikaachana na hiyo kesi na ikanifanya nisiamini tena vyombo vya dola katika kuhakikisha usalama wa mali zetu.Hata baadae nilipotapeliwa shilingi 2,000,000 na kufatilia bado sikupata msaada pia badala yake nilikatishwa tamaa na ofisa upelelezi.

Mifumo mibovu katika mamlaka za kukusanyo mapato.Kwa hali isiyo ya kawaida mamlaka za mapato haswa mamlaka kuu ya mapato hawajali huduma kwa wateja kabisa.Imekuwa kawaida kutumia wiki hadi mwezi kupata huduma ambayo ingechukua siku moja kuipata.Kwa macho yangu nimekuwa nikishuhudia watu wakitoa machozi katika ofisi hizi,si kwa sababu wameshindwa kulipa ila huduma na mifumo mibovu.Mara kwa mara utaambiwa kuna shida ya mfumo hivo hatuwezi kutoa Uthibitisho wa malipo ya kodi au hatuwezi kukupa risiti ya kulipia.Hii inasikitisha sana huku serikali na nchi tunaonekana hatujielewi hata kwenye mambo muhimu kama chanzo kikuu cha mapato yake.

Nashauri mambo haya yafanyike ili kuboresha mazingira ya kujiajiri kwa vijana walio wengi,

Kupunguza mnyororo wa kodi; mfano mfanyabiashara unapaswa kulipa kodi kwa mamlaka kuu ya mapato, tozo ya huduma na usafi halmashauri na leseni ya biashara.Nashauri kupunguzwa kwa kodi na tozo hizi na kurahisisha ulipwaji wake kwa maana kwamba ufanyike kwa pamoja sehemu moja,huku mgawanyo wa hayo mapato ukifanyika kwa mfumo kwa kila mamlaka.Hii itapunguza usumbufu wa kufanya malipo maeneo matatu au manne tofauti.Lakini pia nashauri kuwe na maboresho ufanyaji kazi wa mifumo hii haraka sana kuondoa aibu hii na ikiwezekana malipo yafanyike pasipo umuhimu wa kwenda ofisi husika kwa malipo endelevu ya awamu.

Serikali iweke mazingira salama na bora kujiajiri; Usalama wa mitaji uimarishwe kwa maana ya vyombo vya dola vifanye kazi yake kufatilia maovu kwa ufanisi wa hali ya juu.Kiukweli havijishughulishi kabisa na havifanyi kazi yake ipasavyo inasikitisha pale tunapokuwa hatuko salama kwenye mali zetu na sisi wenyewe.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom