Hasara za ku-bet

Hasara za ku-bet

Wa mbogwe

Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
95
Reaction score
220
ZIFUATAZO NI HASARA ZA KUBET
1. Unadumaa akili unashindwa kuwaza vitu vya maana vyenye kuleta pesa ya uhakika isiyo na mawazo.

2. Ni rahisi sana kupata magonjwa ya moyo ikiwemo presha, kwa wale wanaobet Dau kubwa na hawana bahati ya kushinda.

3. Hata kama utashinda huwezi kuheshimu pesa, kwasababu akili yako itadumaa na kuamini kuwa pesa inapatkana kiurahisi, kwa mtu anaebet ni rahisi sana kucheza hata million ml akiamini itarudi mala nyingi zaidi ya hiyo.

4. Usipokua makini utajikuta umepoteza pesa nyingi bila kujua, mfano chukulia unaBET sh.5000(kwa mda tofauti) kila siku kwa miez mi3 na kufanikiwa kushinda sh.60,000(kwa mda tofauti) je utakua umepoteza shillingi ngapi?

5. Kubet ni KAMALI na imekatazwa na imani zote za dini(ni haram).

6. Huenda kubet kukakufanya kuwa mtumwa wa madeni kwa kuamini kuwa pesa ya kulipa utaipata kwenye kubet, kwa mtu anaebet ni rahis sana kukopa hata laki moja ili aizalishena endapo akiliwa yuko ladhi kukopa tena ili acheze alipe deni na apate pesa nyngne, ndo maana watu wanaobet huwa asilimia kubwa wana madeni(hata madeni ya mitandao pia mfano M-Pawa.

7. Ukizoea kubet huwez kuona fursa zinazokuzunguka.

USHAURI WANGU
* Kama hujawah kubet usijaribu, maana kubet ni zaidi ya addiction.

*Na kama unabet na umeshaliwa zaidi ya pesa uliyowahi kushinda, acha!

MWISHO ........ MWISHO........MWISHO.

Unaweza ongezea pia.
 
Wabongo wanataka kazi soft soft siyo ya kubeba gunia na ukiwahoji watakuambia na ile kodi inayokatwa NAyO haramu
 
Ngoja wazee wa mikeka wakutilie timu.

[emoji16]
 
Na wengi tunaobeti ni wakata ufuta hatujui tunazidi kuwa wakata ufuta,God forbid
 
Kikubwa maslah,kama yakubeba gunia haina maslah ukiringanisha na soft work (kubet) hata wewe usingekubali ukapige hard work yenye maslahi madogo.
 
Mimi sijawahi kubeti na sidhani kama nitafanya hivo,lakini nachoweza kusema ni kuwa kama huna bahati na hayo makitu ni bora kuacha tu.
 
Sijutii kubet,na sintoacha kubet,kama kubet kunaniingizia mara mbili ya mshahara wangu ya nini kuacha?kila mtu na malengo yake
 
Back
Top Bottom