Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Uongozi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) umemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia upya mfumuko wa bei hali ambayo inapelekea ugumu wa maisha kwa wananchi, huku mwenyekiti wa chama hicho Hasheem Rungwe akisisitiza suala la chakula shuleni na hospitali linapaswa kutolewa bure.
Wakiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chama jijini Dar es Salaam wanawake hao wameonesha kilio chao kwa Rais huku wakimtaka awakumbuke na wao kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti wa Baraza Taifa, Fatuma Seleman amesema yapo mambo mengi vanavomuumiza mwanamke wa Kitanzania ukiachilia mbali mfumuko wa bei, amesema hata katika suala zima la uzazi lazima liboreshwe ili wanawake wakimbilie kujifungulia kwenye vituo vya afya na sio nyumbani.
"Chakula kinapaswa kitolewe bure watoto wetu wanaumia ila hawawezi kuongea wanapaswa wapewe ubwabwa bure, hata katika hospitali wagonjwa wapewe bure kwani Serikali inao uwezo kwasababu inakusanya kodi kubwa” amesema Rungwe.
Chanzo: Mwananchi